Hapa ni katika ukumbi wa mikutano hotel ya Empire mjini Shinyanga ambapo leo Jumatano Desemba 21,2016 waandishi wa habari mkoani Shinyanga wamepewa mafunzo kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
Aliyesimama ni katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ili waweze kuandika habari sahihi zaidi kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
Katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael akizungumza.Kulia ni Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner
Mgeni rasmi Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga George Mdoe aliyemwakilisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akifungua semina hiyo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa mbalimbali kuhusu masuala yanayohusu watu wenye ualbino.
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha uoga katika kutoa ushahidi katika kesi za watu wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ualbino
Alisema hivi sasa serikali inahitaji watu wenye ualbino wajumuike katika jamii ndiyo maana baadhi yao wameondolewa katika kambi zao mfano Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kurudishwa katika jamii yao ili kuondoa tofauti yao na watu wengine katika jamii
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akiteta jambo na mwezeshaji katika semina iliyolenga kuwajengea uelewa zaidi waandishi wa habari kuhusu masuala ya watu wenye ualbino, bwana Kadama Malunde,ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu
Semina inaendelea
Bi Nabaggala Edith ambaye ni Mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na masuala ya watu wenye ualbino nchini Uganda (Albinism Support Association Uganda ASAU) akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini Mwezeshaji katika semina hiyo Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu mchango wa vyombo wa habari katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino nchini Tanzania.
Malunde alisema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya watu wenye ualbino kitaifa na kimataifa,kupunguza matukio ya ukataji viungo vya watu wenye ualbino na mauaji, kuelezea juhudi mbalimbali za TAS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Malunde alisema ni kupitia vyombo vya habari hata wadau wamefika nchini na kuchangia kuboresha hali na maisha ya watu wenye ualbino na kufanikisha kuanzishwa kwa siku ya watu wenye ualbino duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 13 kila mwezi Juni
Hata hivyo Malunde alisema bado kuna unyanyasaji wa kijinsia ambapo akina mama waliozaa watoto wenye ualbino wengi wao wamekimbiwa na waume zao,wameachika,wametelekezewa watoto na pia watoto wenye ualbino nao wametekelezwa na kwamba bado kuna mkazo hafifu katika sera na sheria kuhusu masuala ya mauaji ya albino.
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema ipo haja ya kuondoa majina yanayodhalilisha na badala yake itumike "Watu Wenye Ualbino" na siyo maneno mengine.
Afisa programu kutoka Chama Cha Watu wenye ualbino Tanzania,Severin Edward akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akisikiliza hoja kutoka kwa mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akielezea jambo
Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo
Picha ya pamoja
Picha zote na Shinyanga Press Club
No comments:
Post a Comment