Thursday, December 29, 2016

Utulivu wa Mawazo Kupitia Somo la Yoga - Rumadha Fundi

Ufuatao ni muktasari  wa thamani na faida ya kutuliza mawazo ya fikra kuleta amani ya nafsi kupitia mafunzo ya” Meditation” ama  kutafakari katika jamii zetu.

Ulimwengu wa leo wa karne ya 21 unakabiliwa na changa moto nyingi sana kimawazo na maendeleo ya teknolojia kupitia sayansi na njia ya mitandao na kuwawezesha wanaadam kuwa karibu sana ya mitandao kulikoni jinsi ya karne zilizopita.

Uijio huo wa maendeleo ya sayansi, pia umeleta mchanganyiko mkubwa kwenye ubongo wa jamii ya kizazi cha leo na hata kile kilichopita pia, hasa ukizingatia kwamba urahisi wa teknolojia na kuwa na uwezo wa habari na matukio dunia kupitia mitandawazi na hatimae, pia kujenga mazingira magumu kwa wale wasioitumia jinsi inavyostahili.
Yoga Instructor Rumadha Fundi  Katika mkao wa "Gomukhasana" zoezi la Yoga na kutafakari.



Dunia ya kizazi kipya , kina kadiriwa na changa moto za kifra na mawazo, tamaa, nia ya kuwa kama wenzao na taabu ya mawazo katika jamii yetu inayoshawishiwa na hayo maendeleo tuliyonayo sasa. Mambo  kama vile “Stress” na shinikizo la kutaka kuwa  na ushindani katika jamii kumaendeleo  ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyo sababisha hata jamii yetu iwe na msingi dhaifu kulinganisha na vizazi vya karne zilizopita, japokuwa kuna mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, lakini fikra za wengi katika jamii hazina uvumilivu na amani ya mawazo mema katika jamii zetu kutokana na vishawishi vya hayo maendeleo ya nayoletwa na mitandawazi katika viganja vyetu kila sekunde.


Hivyo basi, kutokana na muktasari huu, hapo ndipo haja ya kutuliza mawazo na fikra za ubongo wa mwanaadam ni nguzo muhimu sana katika jamii zetu. Hivyo umadhubuti wa fikra na akili ndio njia pekee inayoweza kutoyumbishwa na vishawishi vinavyo shambulia akili ya mwanaadam mitandaoni kwa nia isiyo elimisha, bali kuujaza ubongo na hali inayo sababisha udhaifu wa mawazo,  kutokuwa na utulivu itumiwapo kwa nia isiyojenga na kuimarisha manufao ya akili na fikra. 

Tafakari “ meditation”, ndio chombo sahihi kupitia mafunzo ya sayansi ya Yoga na mazoezi yake ili kuukabili mazingira na hali halisi ya maisha ya jamii zetu.

Viumbe tumeumbwa na tabaka au safu tano za ubongo zilizo kuwa na mfano wa mauwa ya ndizi na kumenya safu moja hadi nyingine. Utegemea msingi wa elimu ya fikra za mtu mwenyewe kuwa imara. Kila moja ya hizi safu au tabaka zina thamani yake “Subtlety” na uchanga wake “Crudeness” yategemea jinsi gani vikwazo vinavyo kabiri mawazo ya kila mtu binafsi. Hii ndio mifano toka mwili, ubongo na fikra  za mwanaadam na tabia zake. 

“Physical Body” kwa lugha ya Sanskrit :  Annamaya kos’a  ikimaanisha mwili au umbo la viumbe ambayo ni changa sana kimawazo na imeundwa kwa vigawanyo vitano muhimu kimaisha. Kwa mujibu wa sanaa ya yoga, ujulikana kama “ Five fundamental factors”; yaani:

(a)Solid factor  (b)Liquid factor  (c)Luminous factor  (d) Aerial factor  (E)Ethereal factor.
       1.”Conscious or Crude Mind” kwa lugha ya Sanskrit : Ka’mamaya Ko’sa, hii ndio safu yenye kuingoza fahamu au ubongo wa mwanadau kwa maisha ya kila siku na kawaida. Safu hii haina tofauti kimazingira na viumbe wengine kimatendo, kama vile njaa, hamu ya kulala, kuwa na watoto nk. haitofautiani na mnyama.

2.“Subconscoius Or Subtle Mind” Kwa  lugha ya Sanskrit: Manomaya Ko’sa. Hii ni safu inayo tawala safu zote za chini yake na inawajibu  au kazi nne muhimu, yaani 1. Kumbukumbu, 2. Kuwaza, 3. Kusikia uchungu na furaha, na  4. Ndoto. Hizo ndio kazi za hii safu ya ubongo wa mwanadaam. Mifano ya watu wenye hizi sifa ni kama vile; Albert Einstein aleye buni “Theory of Relativity”, Vasily Mendeleev  aliyebuni “Periodic Table”, Charles Darwin aliyebuni “Theory of Evolution & Origin of Species”, Michaelangelo, aliye andika “A seizure of the Soul” na William Blake aliye kuwa “ Visionary Poet and Artist”. Wote wale walioweza penya upeo wao wa fikra katika safu za ubongo wao huendeleza  uwezo wa hali ya juu sana kimawazo kutokana na utulivu wa mawimbi ya fikra zao zinazo watenga na watu wakawaida.

3. “Supramental Mind” Kwa lugha ya Sanskrit : Atima’nasa Ko’sa. Yaani “Akili ya kiwango cha juu sana”.
Hii ni safu au tabaka la ubongo ambapo ubunifu , sanaa na ujuzi wa fikra”Intuition” hutendeka katika safu hii. 

4. “Subliminal Mind” Kwa lugha ya Sanskrit: Vijina’namaya Ko’sa.
Hii ni safu au tabaka la ubongo linalo tawala aina pekee za vipaji. Moja ya vipaji vyake ni kuwa siwa kawaida, utabiri kujuwa ishara ya matokea yajayo na yaliyopo.
Hivyo basi, bila ya kuchambua kwa kina kirefu  moja ya tabaka hizi kwa muktasari tu, njia pekee kuu ya kuiongoza akili ya mwanaadam au mawazo ya mtu, ni kupitia utulivu wa mawimbi ya ubongo kwa njia ya kutafakari na mazoezi ya sanaa ya Yoga. Katika safu hii, subira, utulivu wa mawazo, furaha na maendeleo ya kiroho chimbuko lake lipo hapa.

5. “Subtle Causal Mind”  Kwa lugha ya Sanskrit: Hiran’yamaya Ko’sa.
 Hii ujulikana kama safu au tabaka la dhahabu ”Golden layer”, kutokana na ubora wa kina chake katika ubongo wa mwanadaam. Ni safu mahili yenye kunga’ra na watakatifu wa dini nyingi ni mfano wa ubora wa fikra zao kuwa upeo wa mawazo yao unalingana la safu hii. Miujiza mingi pia utokea mwanaadam anayepenya katika safu kimawazo.

Mazoezi ya sanaa ya Yoga yanaimarisha mawazo na nguvu za mwili kupitia mbinu zake za mafunzo yenye mwigo wa mikao mingi ya wanyama.  Ubongo wa mwanaadam unatoa mawimbi au “Waves,” “Beta waves”  (13 kwa sekunde), Alpha waves”(8 kwa sekunde), Theta waves”(4 kwa sekunde), na “Delta wave” (1 kwa sekunde) mengi na kila safu ina namba ya mawimbi yake na hatimae kufikia uwezo wa kuwa tulivu na kuwa na hizo sifa zilizotajwa hapo juu. 

Haya maelezo yamenukuliwa na mkufunzi wa sanaa hiyo ya Yoga, Rumadha Fundi toka katika jarada la mafunzo ya Yoga “Ananda Sutram” toka kwenye maktaba  ya chuo  alicho soma na kuhitimu sanaa hiyo 1987. “ College of Neo- Humanist Studies”,  Ydrefors, Gullringen, Sweden  na Culcutta, West Bengal, India. 

No comments: