Unakumbuka lile sakata la
mmoja wa wagombea kiti cha Urais nchini Marekani kukumbwa na kashfa ya kutumia
anwani ya barua pepe binafsi kufanya shughuli za Serikali? Au umeshawahi kuona
barua pepe (Pengine unayo unaitumia) ikiwa na mchanganyiko wa herufi na namba,
mfano, wateja wako watajali kweli ukiwa na barua pepe brian255@yahoo.co.tz au brian.mbunde@kampuniyako.co.tz? Sasa Extreme Web Technologies ni mshirika rasmi wa Microsoft kwa upande
wa Tanzania na wanakufahamisha kwamba katika hii ulimwengu tunaoenda nao wa
digitali unapokuwa na professional business
email unajenga uaminifu katika biashara yako na unaonekana uko smart sana.
Pengine bado unajiuliza
“Professional Email” ni nini, ukiangalia mfano hapo juu wa barua pepe ya brian.mbunde@kampuniyako.co.tz inaonesha jina kamili la
mhusika na kuna domain ya kampuni. Hii inamaanisha kwamba hauwafanyi watu waone
jina lingine tofauti na jina lako halisi hivyo kuwapa mitazamo tofauti
linapokuja suala la biashara (Uaminifu) na hapo ndipo Microsoft O365 inakuletea
kile unachohitaji mahali unapokuwa.
Unapataje Barua pepe ya Biashara?
Jinsi ya kupata ni rahisi
sana, unachotakiwa kufanya ni kuwa tu na email na kisha kuwa na “domain” ambayo
imehifadhiwa mahali (server). Baada ya hapo utapewa uhifadhi kumbukumbu
unaofikia 1 TB, kuwekewa Microsoft Office kwenye kompyuta mpakato yako na
kwenye simu yako pia. Huduma nyingine zinahusisha “HD Video Conferencing”.
Kama bado huna uhakika na
umuhimu wa “Professional Email” hizi hapa sababu tano za msingi za kwanini
unatakiwa kuwa na barua pepe maalum kwa ajili ya biashara yako.
1.
Kuonesha Uweledi; “Professional Email”
inaonesha kwamba biashara yako imeimarika na inaendeshwa kwa uweledi wa hali ya
juu, lakini pia inaonesha uko makini na biashara yako na itakuwepo siku zote.
Ukiwa na barua pepe ya kawaida unawapa mashaka wateja kama kweli biashara ni halali
na una uzoefu.
2.
Kujenga
Picha Kubwa; Barua pepe ya kawaida inaweza kuonesha kwamba biashara yako ni
mpya au ndogo. Ukiwa na barua pepe maalum inaleta picha ya kwamba biashara yako
ni kubwa na kuipa muonekano wa kampuni haswa. Pia kutengeneza barua pepe kwa
ajili ya makundi mbalimbali katika biashara yako mfano finance@kampuniyako.co.tz, info@kampuniyako.co.tz, strategy@kampuniyako.co.tz itaimarisha biashara yako.
3.
Kujenga
uaminifu na Imani; Miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la wizi wa
mtandaoni, hivyo wateja wengi huru kutuma taarifa binafsi kwenye barua pepe
kama brian@yahoo.com, lakini unapokuwa na barua
pepe maalum kwa ajili ya biashara yako unampa mteja hali ya kujisikia salama na
uhakika kwa wateja kuwa biashara yako ni halali.
4.
Haina Gharama...Ni Rahisi; Unaweza kuwa na barua pepe
maalum kwa jitihada ndogo tu kupitia mtoa huduma za domain au tovuti bure au
kwa gharama ndogo sana. Faida kubwa ya kuwa na kusajili domain yako ni kwamba
itakuwa pamoja na biashara yako.
5.
Kukuza Biashara Yako; Faida nyingine ya kutumia
barua pepe maalum ni kwamba kila wakati unapowasiliana na mtu/mteja unakuza
biashara yako. Hivyo kama ulikuwa unafikiria barua pepe maalum ni kwa makampuni
makubwa tu, usifikirie hivyo tena.
Kwa Maelezo na taarifa zaidi
tafadhali tembelea http://bit.ly/baruapepeyabiashara au piga simu namba 0784 987363 / 0715 247365 / 022-2127641 au tuma barua pepe kwenda sales@extremewebtechnologies.com
No comments:
Post a Comment