Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kulia) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba.
Kaimu Afisa Utamaduni Mkoa wa Mara Bw. Sheikhdadi Said (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao na Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Mara Bw. Jonson Bambai (aliyesimama) akichangia mada wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.
Mtoa mada kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Richard Ndunguru akitoa mada ya uandishi wa miswada ya filamu na utafiti kwa wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao leo Mkoani Mara.
Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza kutoa mkoa wa Mara wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Mara
Na Genofeva Matemu – WHUSM.
Wanatasnia
wa filamu nchini wametakiwa kutumia fursa zilizopo kikamilifu ili kuifanya
sekta ya filamu kuwa chachu ya maendeleo ya nchi na kuleta ushindani wa kazi za
filamu zinazozingatia ubobezi na
hatimaye kuingia katika soko la ushindani.
Rai
hiyo imetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Nuru Millao wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo
ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.
“Nimatumaini
yangu kuwa mafunzo mnayoyapata hapa yakijumuishwa na fursa mlizonazo za
mandhari mahususi ya upigaji picha katika Mkoa wetu wa Mara, maeneo mazuri na
asilia ya kitalii, utamaduni wetu, maliasili, lugha ya kiswahili na mambo
mengine mengi mkiyazingatia katika uandaaji wa filamu zenu hakika ushindani wa
filamu zetu utakuwa mkubwa sana” amesema Bibi. Millao.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
amesema kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuhakikisha kuwa wadau wanazalisha kazi
bora na hatimaye wanapata mrejesho stahiki kutokana na kazi zao hivyo wadau
walioshiriki warsha watumie fursa waliyoipata kwani warsha imezingatia
ushirikishwaji wa hali ya juu kwa kuwapa wadau fursa ya kuchagia na
kujadiliana.
“Azma ya
Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuhakikisha Tanzania inakuwa taifa la
viwanda hivyo kwa mantiki hiyo, katika warsha hii suala la namna gani tasnia
iimarishwe ikiwa ni pamoja na uwepo wa viwanda vya filamu litatiliwa mkazo
kutokana na hali ya Sekta ya Filamu kuendelea kuimarika kutokana na jitihada za
wadau kwa kushirikiana na Serikali” amesema Bibi. Fissoo.
Naye Katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Mara
Bw. Jonson Bambai amesema kuwa warsha ya mafunzo ya
kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza ni nembo tosha kwa waigizaji wa mkoa wa Mara
kwani itawawezesha kuandaa filamu zitakazowavutia watazamaji kutoka mwanzo hadi
mwisho wa filamu kwa kutumia fursa zilizopo katika mkoa wa mara na kutangaza
upekee wa kabila la wakurya ndani na nje ya nchi.
Tasnia
ya filamu imeendelea kuwa chombo muhimu sana kinachochangia katika Maendeleo ya
Taifa. Sote tutakubaliana kuwa ile dhana ya awali kuwa filamu ni chombo cha
kutoa burudani tu imeanza kufutika kufuatia sekta hii kutoa ajira kwa makundi
mbalimbali na kuchangia katika uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment