Tuesday, December 13, 2016

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAFANYA USAILI KUWAPATA WARATIBU NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI, ZANZIBAR LEO

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti cha Usaili wa Waratibu na Wasimamizi Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani, Zanzibar utakaofanyika Januari 22, 2017.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume wakati wa kikao cha Usaili wa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjata.
  Baadhi ya Wajumbe wa Seckretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakifuatilia kwa makini zoezi la Usaili wa kuwapata Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipitia vyeti na nyaraka mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Usaili wa nafasi ya Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.
 Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Mratibu wa Mkoa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bw. Salum Juma Mgunya akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini Zanzibar.
 Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Msimamizi wa Uchaguzi  katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bi. Fatma Gharib Haji akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini
Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia Usaili wa Wasimamizi na Waratibu wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar. Picha na Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

No comments: