Saturday, December 3, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 3.12.2016


DCP AHMED MSANGI KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

§  KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI AINA YA AK 47, BASTOLA 1, BOMU LA KUTUPA KWA MKONO 1, NA VISU NA JAMBIA NA KUUAWA NA WATU WAWILI WAZANIWAO KUWA NI MAJAMBAZI. 

KWAMBA BAADA YA MATUKIO YALIYOTOEA HIVI KARIBUNI HAPA JIJI MWANZA, MSAKO MKALI NA UPEPELEZI ULIANZA KUFANYIKA. AIDHA WAKATI ASKARI WAKIENDELEA NA MSAKO WA WAHALIFU PALITOKEA TUKIO LA KUJERUHI KWA KUTUMIA SILAHA TAHERE 30.11.2016 MAJIRA YA SAA 15: 00HRS ENEO LA MGAWAHA UITWAO DINNERS AMBAPO WATU WAWILI WALIJERUHIWA.

HATA BAADA YA TUKIO HILO ASKARI WALIENDELEA KUFUATILIA NDIPO KULIAPTIKANA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI WETU NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WANNE NA KUHOJIWA VIZURI  AMBAO 1. RAJABU ABDALLAH @ WABAYA WATU MIAKA 27 MUENDESHA PIKIPIKI, 2. EMILY TIMOTHEO, 3.BAKARI MASOUD @ BEKA, NA 4. GEOFREY PETRO JOHN, MNAMO TAREHE 2.12.2016 MAJIRA YA SAA 12:00HRS, WATUHUMIWA HAO WALIPOFANYIWA MAHOJIANO WALIKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YALITOKEA HIVI KARIBUNI YA ; ENEO LA MTAA WA NKURUMAH AMBAPO WALIVAMIA DUKA LA BIDHAA MBALIMBALI NA MIAMALA YA FEDHA NA KUUWAA MWANAMKE MMOJA MWENYE ASILI YA KIHINDI.

PIA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA KUUA MCHINA  LILILOTOKEA HIVI KARIBUNI KATIKA MTAA WA MAHINA ALLIANCE AMBAPO  PIA WAALIPORA FEDHA NA TUKIO WALILOVAMIA MGAHAWA UITWAO DINNERS ULIOPO BARABARA YA KENYATTA AMBAPO WATU WAWILI WALIJERUHIWA LAKINI HAWAKUWEZA KUCHUKUA FEDHA. WATUHUMIWA HAO WALIELEZA PIA  WANAZO SILAHA TATU (3), KUBWA MBILI NA NDOGO MOJA, PIA WALIWATAJA WENZAO WAWILI AMBAO BADO TUNAWATAFUTA.

WATUHUMIWA HAO WALIKUBALI KUTOA USHIRIKIANO KWA ASKARI  KUHUSU ENEO WALIPOFICHA SILAHA, WALIDAI SILAHA MBILI ZIPO MAFICHONI BUHONGWA NA MOJA IPO KWA MWENZAO AMBAE BADO HAJAKAMATWA, TAREHE 2.12.2016 MAJIRA YA 23:00HRS USIKU ASKARI WALIKWENDA HADI ENEO LA BUHONGWA “B” MAARUFU KWA JINA LA MSITU WA DEO AMBAPO WALIDAI ZIPO MAENEO HAYO.

WAKATI WATUHUMIWA WALIPOKUWA WANAELEKEZA ASKARI MAHALI WALIPOFICHA SILAHA, WALIKURUPUKA NA KUANZA KUKIMBIA WOTE WA NNE SEHEMU MBALIMBALI KWA KUSUDI LA KUTOROKA, ASKARI WALIFYATUA RISASI HEWANI KUWAZUIA LAKINI HAWAKUSIMAMA NDIPO ZILIWALENGA WATUHUMIWA WAWILI AMBAO 1. RAJAB ABDALLAH NA 2. EMILY TIMOTH, SEHEMU ZA MIKONONI, MIGUUNI NA KIUNONI NA KUFARIKI DUNIA WAKATI WAKIPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA MATIBABU, HUKU WENGINE WAWILI WAKIFANIKIWA KUTOROKA LAKINI WAKIWA NA MAJERAHA.

ENEO LA TUKIO LILIZUNGUKWA NA ASKARI USIKU WOTE PAMOJA WANANCHI HADI KUNAPMBAZUKA ASUBUHI YA TAREHE 03.12.2016, ILI KUWEZA KUBAINI KAMA KUTAKUWEPO NA WATU WALIO JERUHIWA NA RISASI AU SILAHA ZILIZOTELEKEZWA, NDIPO ZILIPATIKANA SILAHA MBILI, MOJA AINA YA SMG NA MAGAZINE MBILI MOJA IKIWA NA RISASI 30, NYINGINE RISASI 15 NA SILAHA NDOGO AINA YA BASTOLA, AMBAPO NAMBA YA SILAHA HIZO ZILIKUWA ZIMEFUTIKA, LAKINI IMEGUNDULIKA WATU HAWA WALIKUWA WANAENDESHA PIKIPIKI, HAIJAFAHAMIKA KAMA NI ZA KWAO AU WAMEAJIRIWA AU DEIWAKA, MIILI YA MAJAMBAZI HAO IPO HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI.

AIDHA KULIPATIKANA PIA TAARIFA ZA UWEPO WA WKIKUNDI CHA WATU WENYE UHUSIANO NA KIKUNDI CHA MAJAMBAZI  WALIOUWA NA ASKARI KATIKA MILIMA YA UTEMEINI MKOLANI  MWAKA HUU, WENYE SILAHA KUBWA NA NZITO, ASKARI WALIENDELEA NA UFUATILIAJI KWA KUSHIRIKINA NA ASKARI WENZETU  KUTOKA MAKAO MAKUU.

KATIKA UFUATILIAJI WA TAARIFA HIZO MNAMO TAREHE 02.12.2106 MAJIRA YA 21:30HRS ASKARI WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA AMBAYE JINA TUNALIHIFADHI KWA SABABU ZA KIUCHUNGUZI (UFUATILIAJI BADO UNAENDELEA), ALIPOHOJIWA NA ASKARI ALIKIRI KUWA WANAZO SILAHA NYUMBANI KWAO ANAPOISHI MAENEO YA KISHIRI BUKAGA.

MTUHUMIWA ALIWAPELEKA ASKARI HADI NYUMBANI KWAO, PALIKUWA NA GIZA LAKINI KULISIKIKA SAUTI ZA WATU WALIOKUWA WAKIONGEA NDANI YA NYUMBA HIYO. ASKARI WALIZINGIRA SEHEMU ZOTE NA KUINGIA NDANI YA NYUMBA HIYO, WAKATI WANAINGIA NDANI ALICHOMOKA MTU MMOJA ALIYERUSHA KITU KAMA JIWE  NA KUFANIKIWA KUKIMBIA AMBAPO ASKARI WALILICHUNGUZA NA KUGUNDUA KUWA LILIKUWA NI BOMU LA KUTUPA KWA MKONO BAHATI NZURI LAKINI HALIKUWEZA KULETA MADHARA (HALIKULIPUKA).

ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WOTE WALIOKUWEPO NDANI YA NYUMBA HIYO LAKINI MMOJA ALIFANIKIWA KUTOROKA AMBAYE NI YULE ALIYERUSHA BOMU LA MKONO, AIDHA WALIFANYA UPEKEKUZI KWA KUSHIRIKAINA NA MWNYEKITI WA MTAA HUO NA KUFANIKIWA KUKAMATA SILAHA AINA YA SMG AMBAYO NAMBA ZAKE ZIMEFUTWA, MAGAZINE TANO ZENYE JUMLA YA RISASI 150, VISU VIWILI, JAMBIA MOJA, RISASI MBILI ZA SILAHA AINA YA MARK IV, BOMU LA KUTUPA KWA MKONO NA KOFIA MOJA YENYE MUONEKANO SAWA NA KOFIA ZA JESHI (KOMBATI).

JUMLA YA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILI NI 18, AIDHA WAPO WATOTO WADOGO 12 WENYE UMRI USIOZIDI MIAKA KUMI NA MINANE, PIA WAPO WANAWAKE WAWILI, NA WANAUME WATU WAZIMA WA NNE, UFUATILIAJI NA UPELEZI WA KUWASAKA WATUHUMIWA WENGINE  BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTULIA NA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA POLISI MAPEMA ILI ZIWEZE KUFANYIWA KAZI KABLA UHALIFU HAUJATOKEA.  ANATOA WITO PIA  KWA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KUPANGISHA KUWA MAKINI NA WATU WANOWAPANGISHA KATIKA NYUMBA ZAO, LAKINI PIA KWA WAMILIKI WA PIKIPIKI KUWA MAKINI NA WATU WANAO WAAJIRI KWANI WAPO WATU AMBAO SIO WAAMINIFU.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments: