Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na
wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
jijini Dar es Salaam Leo.(Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Joakim Mhagama )
kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya
Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam
Leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akionesha kwa wadau mbalimbali Mpango Kazi wa
Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi nakala ya Mpango Kazi wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya baada ya uzinduzi wa Mpango Kazi
wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe
akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla
ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na
Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.
Charles Mwijage akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango
Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Joakim Mhagama akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa
Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Alvaro Rodriguez akiongea na wadau
(hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
jijini Dar es Salaam Leo.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mh. Anastazia Wambura akiongea na wadau
(hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
jijini Dar es Salaam Leo.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo
Mh. Anastazia Wambura (kulia) akifurahia jambo na kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Injinia Stella Manyanya baada ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
jijini Dar es Salaam Leo.
Na Eliphace Marwa – Maelezo
13/12/2016
SERIKALI imezindua Mpango
Kazi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga
kushirikisha wadau wengine katika jitihada jumuishi za kuzuia ukatili
dhidi ya wanawake na watoto na hivyo kusaidia wahanga wa ukatili huo
kupata huduma stahiki ili kudhibiti ukatili nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa niaba ya
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa jamii inajukumu la
kuhakikisha ukatili wa wanawake na watoto unapigwa vita kwa vitendo.
“Serikali
inaikumbusha jamii kupambana na vitendo vya ukatili kwani ukatili
unafanyika kuanzia ngazi ya familia hivyo ni jukumu la wananchi kutoa
taarifa za ukatili wa wanawake na watoto ili vyombo vya dola viweze
kuwachukulia hatua za kisheria”, alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa Kumekuwepo
na matukio mengi ya ukatili yanayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na umaskini katika familia, mila na desturi potofu zenye
athari katika jamii, malezi na makuzi mabovu na sheria kandamizi.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Asasi za Kiraia zinazoshughulika na utetezi
wa haki za watoto (TCRF) Bw. Erick Guga amesema kuwa watoto ndiyo
wahanga wakubwa wa ukatili huu hivyo ni wakati muafaka kwa mpango kazi
kuanza kazi ili kuwanusuru wanawake na watoto katika ukatili.
“Mpango
Kazi huu wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini
Tanzania utakuwa ndiyo dira kwa wadau wote wa masuala ya maendeleo ya
wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vema Serikali kushirikiana na
wadau kila inapohitajika”, alisema Bw. Guga.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba
Nkinga amesema kuwa, kabla ya kuandaliwa kwa Mpango Kazi huu, Tanzania
ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake
na watoto.
Aidha
Bi. Sihaba ameongza kuwa mipango hiyo haikuwa na mfumo wa pamoja wa
kufuatilia na kutathmini ufanisi unaopatikana. Vilevile, kutokana na
madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maendeleo ya nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi wanachama waliazimia kwa
pamoja kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.
“
Tanzania ni kati ya nchi nne (4) za kwanza duniani na nchi pekee katika
Afrika iliyowezeshwa kupitia jukumu lilioanzishwa la kusaidia nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa kuandaa mpango wa kuzuia na kuitikia afua
za kudhibiti ukatili ili kuwa na mipango thabiti ya upatikanaji wa haki,
usawa na maendeleo kwa wote”, alisema Bibi.Sihaba.
Akieleza
katika uzinduzi huo Mkurugenzi Sera na Mipango Emmanuela Achayo
aliseama kuwa Mpango kazi huo wa aina yake una maeneo makuu manane (8)
yatakayotekelezwa na wadau wa maendeleo ya wanawake na watoto.
“Maeneo
hayo ni kuimarisha uchumi wa kaya, Uzuiaji wa mila na desturi zenye
madhara na Uboreshaji wa mazingira salama katika jamii”, alisema Achayo.
Maeneo
mengine ni Kuendeleza mazingira salama ya mafunzo shuleni na stadi za
maisha na kuhuisha mahusiano, malezi na makuzi katika familia,
Utekelezaji na usimamizi wa sheria, Utoaji huduma kwa wahanga na
Uratibu, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa miaka
mitano kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 20121/21022.
Mpango
huu mahususi unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa baada ya miaka mitano
ya utekelezaji kwani utawezesha kuondoa ukatili dhidi ya wanawake kwa
asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022; na Kuondoa ukatili dhidi ya watoto
kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022, na hivyo kuleta mabadiliko
makubwa kwa kuwa na familia salama, na jamii yenye utulivu.
Kazi
zitakazotekelezwa na kila mdau kuanzia familia, jamii, halmashauri,
mikoa, wizara, sekta binafsi, asasi za Kiraia na wabia wa maendeleo
Mpango umeweka mfumo fungamanishi wa uratibu, ufuatiliaji na tathmini
ambao utaratibiwa katika ngazi ya Taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ngazi
ya mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, na ngazi ya halmashauri na
Wakurugenzi Watendaji.
No comments:
Post a Comment