Waziri
wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya
Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA),
Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce
Shaidi.
Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
Katika hafla ya kufungua kituo hicho nyama choma zilikuwepo ingawa mimi sikubahatika kupata walau finyango moja.
Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na
wageni waalikwa.
Waziri
wa Fedha, Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi
wengine akitoka kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani
kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa bodi ya NBAA na Mfuko wa GEPF
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa
hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC),
kilichopo Bunju na Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es
Salaam leo.
"Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.
Mpango
alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali
kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi
zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.
"Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.
Aliwataka
wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika
kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao
kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.
Mpango
alisema kuwa serikali itaendelea kuwatumbua watumishi wasio waaminifu
na wahasibu bila ya kumuonea muhusika huruma na kuwa atakayebainika
atapelekwa mahakama ya mafisadi iliyofunguliwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa NBAA Pius Maneno alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita
walikuwa wakitumia sh. biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia
kumbi hivyo ujenzi wa kituo hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa
kitakuwa ni chanzo cha mapato.
Mwenyekiti
wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa
mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko
wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.
Alisema
awali walikadiria ujenzi huo ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14
lakini kutokana na sababu mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh.
bilioni 33 zaidi ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.
Mwenyekiti
wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi aliishukuru serikali kwa ushirikiano na
mifuko ya jamii na NBAA hasa katika suala zima la kusukuma maendeleo ya
nchi ikiwa na kuzitaka taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho
cha kimataifa ili kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.
No comments:
Post a Comment