Frank Mvungi-Maelezo
Kuelekea
Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Serikali imepongezwa kwa Mafanikio
yaliyofikiwa katika kipindi chote tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya
tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wakati
wa mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka hamsini na tano ya
Uhuru yanayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 9 Desemba mwaka huu.
“Tumepiga
hatua kubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile
elimu,Afya,Maji,usafirishaji na miundo mbinu ukilinganisha na wakati
tunapata Uhuru” Alisisitiza Chongolo
Katika
Sekta ya elimu Chongolo anabainisha kuwa Serikali katika awamu zote
tangu awamu ya kwanza hadi sasa zimekuwa zikiweka kipamaumbele katika
Sekta hiyo hali iliyochangia kuongezeka kwa shule za msingi ,Sekondari
na Vyuo Vikuu .
Akifafanua
zaidi Chongolo ameongeza kuwa elimu bure ni miongoni mwa dhamira ya
Serikali ya Awamu ya tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuzidi
kuendeleza azma ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ya kupamabana na maudui watatu ambao ni ujinga,maradhi na
umasikini.
Akizungumzia
kuhusu miundo mbinu ya barabara anabainisha Tanzania ya sasa ina
tofauti kubwa na wakati Taifa lilipokuwa likipata Uhuru ambapo barabara
za lami na madaraja yalikuwa machache lakini hivi sasa Mikoa yote
inafikika kwa urahisi.
Anaongeza
kuwa sekta ya maji pia imeimarika ukilinganisha na wakati wa uhuru
ambapo moja ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na Serikali ni mradi wa
maji wa ziwa Victoria hadi shinyanga na mwingine ni ule wa upanuzi wa
mitambo ya Ruvu juu na Ruvu Chini ambayo imeanza kumaliza tatizo la maji
katika Jiji la Dar es salaam.
Aidha
Chongolo aliwaaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa
rasilimali za Taifa na miundo mbinu iliyopo kwa maslahi ya taifa kwa
kuwafichua wale wote wanaokwaamisha au kuhujumu nia njema ya Serikali
katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Sherehe
za Uhuru huadhimishwa kila mwaka inapofika tarehe 9 mwezi Desemba
ambapo mwaka huu Kitaifa zitafanyika Jijini Dar es salaam na Kuongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
mara ya kwanza tangu achaguliwe mwaka mmpja uliopita.
Kauli
mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga
Rushwa,Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo yetu.”
No comments:
Post a Comment