Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(wa pili kulia) akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Mauritius pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni Mhe. Santaram Baboo (wa kwanza kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Sanaa na Utamaduni.Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Mauritius kuhusu kuimarisha sekta ya Sanaa na Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo (wa kwanza Kulia) akizumgumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa majidiliano ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyesimama) akiongea jambo wakati wa mazungumzo kati ya Wizara yake na Serikali ya Mauritius katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo baada ya mazungumzo baina yao kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake na viongozi wa Serikali ya Mauritius baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment