Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa
mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati ya Kigeraetuma
iliyopo Kijiji cha Kamuguruki, Musoma Vijijini ikiwa ni zawadi ya sikukuu ya
Krismasi.
Zawadi
hiyo imetolewa leo kijijini humo katika hafla ya chakula aliyoiandaa kwa
ajili ya wananchi wa Kijiji hicho pamoja na vijiji vingine mara baada ya
ibada iliyofanyika katika kanisa la Menonite lililopo kijiji cha
Nyakatende, Musoma Vijijini..
Katika
hafla hiyo Profesa Muhongo aliongozana na familia yake pamoja na rafiki zake
kutoka Ujerumani ambao kwa pamoja walijumuika na wananchi wa Musoma vijijini
kusherehekea.
Kanisa
la Menonite la kijiji cha Nyakatende ambapo Mbunge wa Musoma Vijijini
na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, familia yake
na rafiki zake kutoka Ujerumani walishiriki ibada ambapo aliahidi
kuchangia ujenzi wake.
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (wa tatu kutoka kushoto waliokaa katika viti) katika picha ya
pamoja na waumini wa Kanisa la Menonite mara baada ya kumalizika ibada.
Diwani
wa Kata ya Nyakatende, Rufumbo Rufumbo (katikati) akionesha vifaa vya
umeme jua alivyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) .
Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (aliyeshika kipaza sauti) akiwa amepanga foleni na
wananchi wa jimboni mwake kwa ajili ya kuchukua chakula.
Wananchi wa Kata ya Nyakatende wakichukua chakula
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (wa pili kulia) akionesha vifaa vya umeme jua ambavyo Balozi wa
Korea nchini anatarajiwa kupeleka mtaalamu jimboni humo ili kuwafundisha
vijana namna ya utengenezwaji wake ili kujipatia kipato
No comments:
Post a Comment