Friday, December 23, 2016

MWANA DAR ES SALAAM SHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMAS KWA NAMNA HII

Na Jumia Travel Tanzania
JUMAPILI hii ya Desemba 25 ni sikukuu ya Krisimasi ambapo wakristo nchini wataungana na wenzao duniani katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bwana wao Yesu Kristo.
Kwa kawaida sikukuu hii husherehekewa kwa watu kujumuika na familia zao ambapo hukusanyika kwa pamoja nyumbani, kusafiri, kufurahia chakula, vinywaji, kupeana zawadi pamoja na burudani nyinginezo walizoziandaa.
Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukupendekezea namna mbalimbali nyingine tofauti na ulizozizoea za kufurahia sikukuu hii mashuhuri duniani na kuifanya iwe ya kuikumbuka zaidi katika maisha.
yako.
Ipeleke familia yako kwenye Seafood Gala
Siku ya Krisimasi bendi ya Skylight itakuwa pale kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kusherehekea sikukuu ya Krisimasi. Litakuwa ni tukio zuri kwani litajumuisha shughuli tofauti zitakazolenga kila rika kama vile vyakula vya baharini, michezo ya watoto, muziki wa bendi na kutoka kwa ma-DJ maarufu jijini Dar es Salaam.  
Washuhudie kwa mara ya 
kwanza WCB kwenye jukwaa moja
Pengine hili ni tamasha kubwa la kufungia mwaka ambalo lililokuwa likisubiriwa na mashabiki wengi wa muziki nchini. Mwanamuziki maarufu na mwenye mafanikio zaidi nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla anatarajiwa kudondosha burudani ya aina yake akiwa na wasanii waliomo kwenye lebo yake ya muziki ya WCB ambao ni Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko na Queen Darleen. Tamasha hilo limepewa jina la ‘Wasafi Beach Party’ na linatarajiwa kufanyika siku ya Desemba 24, 2016 katika hoteli ya nyota tatu ya Jangwani Sea Breeze Resort ambapo tayari kuna orodha ya wasanii na watu maarufu kadhaa tayari wamethibitisha kuwepo.  
Nenda kafurahie bufee la maana kwenye mgahawa unaozunguka wa Akemi
Jaribu kuinogesha Krisimasi hii kwa kwenda kufurahia chakula kwenye mazingira tofauti na nyumbani. Akemi ni mgahawa pekee unaozunguka nchini Tanzania ukiwa unapatikana kati ya majengo marefu jijini Dar es Salaam, Golden Jubilee Tower, ikikupatia fursa ya kujionea jiji hilo ukiwa ghorofani huku ukifurahia vyakula, vinywaji, muziki na mazingira tulivu na ya kifahari ukiwa pale.
Double Tree Hotel watakuwa na Festive Fun
Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam ambayo unaweza kuipata kupitia mtandao wa Jumia Travel (www.travel.jumia.com), inapatikana katika mazingira tulivu pembezoni mwa kitongoji cha Msasani ambapo utaweza kufurahia mandhari nzuri ya bahari pamoja na bustani nzuri. Kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu za Krisimasi, Boxing Day mpaka Mwaka Mpya wameandaa ‘Festive Fun’ yenye ofa kadha wa kadha za vyakula, vinywaji na muziki mzuri wa disco la nguvu la kukuburudisha.
Tembelea majumba ya sinema
Wewe kama ni mpenzi wa filamu basi sikukuu hii itaenda vizuri kwako kwani kutakuwa na filamu mpya na kali ambazo zinatoka kipindi hiki. Filamu hizo ni kama vile Assassin’s Creed, Passengers na Why Him? Majumba ya filamu kwa hapa nchini ya Century Cinemax yanapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam (Mlimani City,
Dar Free Market Oyster Bay na Mkuki House Mall) na Arusha hivyo unaweza kuyatembelea ili kuzifaidi katika kipindi hiki.
Sikukuu ni kipindi muhimu sana cha kufarahia kwa amani na utulivu, Jumia Travel inakusihi kusherehekea kwa uangalifu ili usijiingize kwenye matatizo kwani kipindi hiki vyombo vya dola vinakuwa makini zaidi kwa wale wote watakaotumia kisingizio cha sikukuu kuvunja sheria zilizowekwa.

No comments: