Friday, December 23, 2016

MUNGAI ASAIDIA YATIMA IRINGA MISAADA YA TSH MILIONI 4.5 KWA AJILI YA SIKUKUU YA KRISMAS

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto ) na mfanyabiashara Geofrey Mungai wakiwa wamewapakata watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa waliokuwa wametupwa na wazazi wao na kuchukuliwa na kituo hicho jana wakati Mungai alipofika kukabidhi chakula na nguo za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa watoto hao 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela akisalimiana na Geofrey Mungai kulia 

Bw Mungai akiwa na mmoja kati ya watoto yatima wanaolelewa kituo cha DBL 
Viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha DBL kutoka kushoto ni mkurugenzi wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe , mfadhili Geofrey Mungai , katibu wa CCM Iringa , mwenyekiti wa CCM Iringa mjini , mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela,mbunge viti maalum Iringa Ritta kabati ,diwani Dolla Nziku 

Mtoto wa mbunge Mwamoto Leah akitoa ahiadi yake ya Tsh 50000 kwa ajili ya kusaidia yatima 
katibu wa CCM Iringa mjini akiahidi kuchangia yatima hao 
Mbunge Kabati akiahidi kuchangia Tsh 500,000 kwa ajili ya Yatima haoNa MatukiodaimaBlog .
WATOTO yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa na wale wa kituo cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa Iringa wapewa msaada wenye nguo na chakula msaada wenye thamamani ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya .

pamoja na msaada huo wa chakula na mavazi pia Mungai aliahidi kuchangia Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki katika kituo hicho na kufanya msaada wake kufikia Tsh milioni 4.5 


Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kumshukuru mfanyabiashara huyo kwa kukumbuka yatima bado ametoa onyo kali kwa wanawake wote wanaotupa watoto kuwa ikibainika watachukuliwa hatua kali .


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Geofrey Mungai alisema imekuwa ni kawaida ya familia yake kila mwaka kusherekea sikukuu mbali mbali pamoja na watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.


Mungai alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.


Hata hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.


Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.


Hivyo alisema kwa mwaka huu amelazimika kutoa msaada wa nguo na chakula kwa kila kituo msaada wenye thamani ya Tsh milioni 1.5 na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa ajili ya watoto hao ili siku ya sikukuu nao waweze kufafana na watoto wengine ambao wanawazazi wao wote wawili .


Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe Bw. Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa kituo chake cha DBL kilichopo chini ya usimamizi wa mchungaji Neema Mwaisumbe kina watoto yatima 43 na kuwa maendeleo ya kituo hicho yametokana na jitihada za wadau mbali mbali ambao wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho.


Alisema kuwa mbali ya familia hiyo ya Mungai kuendelea kutoa msaada wakati wa sikukuu mbali mbali kwa watoto hao bado michango yake imeendelea kuwa chachu kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto hao kwa misaada mbali mbali .


Hata hivyo alisema kuwa wadau wanaoendelea kusaidia kituo hicho ni wengi zaidi na kuwa kwa umoja wao kituo hicho kinaendelea kuthamini michango yao na kuomba kuzidi kujitolea zaidi kwa ajili ya watoto hao kwa ajili ya kuona watoto hao wanapata elimu Kituo hicho ambacho kina zaidi ya miaka 15 15 toka kuanzishwa kwake kimefanikiwa kuanzisha shule yake ya Sekondari iliyopo kijiji cha Mgera ambayo inapokea na watoto wengine kwa kuchangia ada ndogo zaidi kuzindua shule ya sekondari .


kama umeguswa na jitihada za wale wote wanaojitolea kusaidia yatima wa kituo hiki cha DBL mkimbizi Iringa unaombwa kuchangia mchango wako wowote kupitia namba hii ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hiki mchungaji Mpeli kupitia huduma ya TIGO PESA 0719239936 na M-PESA ni 0754362536 na Mungu atakubariki na kukuongezea pale ulipopunguza.


Aidha alishukuru ushirikiano kubwa ambao umekuwa ukionyeshwa na wadau mbali mbali kama mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu ambae amekuwa akijitolea kusomesha baadhi ya watoto elimu ya msingi kwenye shule yake ya Star pia mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na wadau wengine mbali mbali .


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Kasesela alisema kuwa hatapenda kuona katika wilaya yake watoto wanaendelea kutupwa ama kutelekezwa na wazazi wao baada ya kuzaliwa na kutaka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wale wote wanaotupa watoto .


Mkuu huyo wa wilaya kwa kushirikiana na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa ajili ya kuungana na Mungai kusaidianbsp; watoto hao walichangia Tsh milioni moja 

No comments: