Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene, akisalimiana na
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, baada
ya kuwasili Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufunga mafunzo ya
uongozi na maadili ya vijana wazalendo 47 yalifungwa chuoni hapo Dar es
Salaam leo. Kulia ni Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa
Taifa ambaye alipata fursa ya kuzungumza katika hafla hiyo kuhusu suala
zima la maadili ya uongozi na uzalendo.
Kikao kifupi kikifanyika ofisini kwa mkuu wa chuo hicho
kabla ya kwenda ukumbini.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa ukumbini kwenye hafla hiyo.
Mgeni
rasmi Waziri Simbachawene (wa pili kushoto) na viongozi wengine
wakielekea ukumbini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbert
Sanga, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam,
Ramadhan Madabida, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama na Mkuu wa
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Taswira ya ukumbi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbert Sanga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza.
Mzee Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wahitimu hao 47 wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wahitimu hao 47 wakiimba wimbo maalumu.
Waziri Simbachawene akihutubia.
Muhitimu, Ebeneza Emmanuel akipokea cheti kutoka kwa
mgeni rasmi.
Petro Magoti akikabidhiwa cheti.
Mhitimu Happiness Agathon akipokea cheti.
Mzalendo Theodora Malata akipokea cheti.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja na wahitimu hao.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amesema ili
kusimamia mabadiliko na maendeleo ya nchi na maadili inatakiwa kuwa na
kiongozi mbabe na mtemi.
Simbachawene
aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi na maadili kwa
wahitimu 47 wazalendo waliyoyapata Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu
Nyerere Kivukoni Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi
ya ujenzi ya kujitolea ya mwezi mmoja wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema
ili kusimamia mabadiliko na maendeleo nchi inatakiwa kuwa na mtu mbabe
na mtemi na si kutegemea kundi fulani la watu kwani kwa kufanya hivyo
kila kundi litahitaji kupendelewa baada ya kujiona bora kuliko jingine.
Alisema
bila kuwa na viongozi wenye maadili nchi haiwezi kusonga mbele kwani
tangu kuachwa kwa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako
kulikuwa kukitolewa mafunzo ya maadili athari zake zilijitokeza na
ndipo kwa kipindi cha miaka 20 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijikuta
kikivamiwa na matajiri wakitaka nafasi mbalimbali za uongozi katika
ngazi za ubunge, urais na kuingia katika ujumbe wa mkutano mkuu wa chama
kwa njia ya fedha.
“Napenda
kusema kuwa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kukifumua chama chetu hasa
katika mfumo mzima wa kupata viongozi kwani uliopo umetufanya tupoteze
baadhi ya nafasi katika majimbo na hata katika uchaguzi ndogo kutokana
na mfumo mbaya tulishindwa vibaya baada ya wanachama wetu kumpigia kura
mtu mwingine kwa hasira huko vikao vyote vikiendeshwa kwa misingi ya
fedha” alisema Simbachawene.
Alisema
ilifika kila jambo lilikuwa haliwezi kufanyika bila ya kuomba ufadhili
kutoka kwa matajiri ambao wengi wao ndio hao walikuwa wakwepa kodi.
Aliongeza
kuwa watumishi wa umma wamekuwa wakilalamika kuwa hali ya maisha
imekuwa ngumu huku wengine wakisema hazina hakuna fedha wakati hakuna
hata mwezi mmoja ambao mtumishi amekosa kupewa mshahara wake.
Alisema
pengine hali hiyo inatokea kwa kuwa watumishi hao walikuwa wakitegemea
kitu kingine mbali ya mshahara baada ya mianya hiyo kufungwa ndio maana
wameanza kulalamika.
Simbachawene
alisema awali bandarini kulikuwa na pilika pilika nyingi mlundikano wa
mankotenta na magari lakini makusanyo yalikuwa hayafiki hata bilioni
moja kwa mwezi lakini hivi sasa pilika pilika hizo hazipo tena makusanyo
yanafikia trioni moja hii inaonesha pamoja na kuwepo kwa pilika pilika
hizo kodi ilikuwa hailipwi ipasavyo.
Alisema
nchi ilifikia pabaya kwani kila sehemu kulikuwa na madalali iwe
hospitali, ofisi za serikali, mahakamani na hata kupata cheo lakini hivi
sasa mambo hayo yamebanwa.
Alisema
anachokifanya Rais John Magufuli ni mabadiliko ili watu waache kuishi
kwa mazoea badala yake wafanye kazi ili nchi ipige hatua katika masuala
yote.
Simbachawene
alisema changamoto kubwa iliyopo ni kuchanganya sera za siasa na za
uongozi jambo linalosabisha mambo mengine kushindindwa kusonga mbele.
Waziri Simbachawene aliwapongeza wahitimu hao kwa kuwa na uzalendo kwa nchi yao ambapo aliahidi majina yao kuyapeleka kwa Rais Dk. John Magufuli kuona jinsi ya kuwasaidia ukizingatia kuwa wote ni wasomi wa shahada ya kwanza katika ngazi ya taaluma mbalimbali na akawaomba vijana wengine kuiaga mfano wa vijana hao.
Mkuu
wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila
alisema baada ya kuona mmomonyoko wa maadili miongoni mwa jamii ya
watanzania hasa kwa baadhi ya viongozi chuo hicho kimeona ni vyema
kurejesha tena mafunzo ya uongozi na maadili ili kupitia mafunzo hayo
waweze kupunguza kama si kumaliza kabisa kasi ya mmomonyoko wa maadili
iliyopo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment