Saturday, November 19, 2016

NEC YAZIONYA ASASI ZINAZOTAKA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (wa pili kushoto) wakati kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe.

Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akieleza jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na katikati ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge vitabu vya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchgauzi wa Rais,Wabunge na Madiwani baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga kura.

Hussein Makame, NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia debe sera za chama fulani cha siasa kwani kufanya hivyo kukiuka matakwa ya Kisheria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stela Manyanya alitaka kufahamu Tume ina utaratibu gani kuhakikisha baadhi ya Asasi zinazofadhiliwa kutoa elimu ya mpiga kura kutumia nafasi hiyo kuhasisha sera za chama fulani.

Bw. Kawishe alisema Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa.

“Tume ikishatoa kibali inafanya ufuatiliaji na tathmini.Tumekwambia nenda katoe elimu ya mpiga kura..lazima tutafuatilia ili kuona kwamba unachotakiwa kusema ndicho.Lakini kwa sababu tu umetoa uchochezi Tume ndiyo imekupa kibali na Tume ndiyo yenye mamlaka ya kukunyima icho kibali” alisema Bw. Kawishe na kuongeza:

“Kwa hiyo kwa kuwa Tume haina uwezo wa kifedha inaruhusu Asasi zijitegemee lakini zikishaenda kwenye siasa tutazinyia icho kibali na kibali kitafutwa kwa sababu Tume ina mamalaka hayo Sheria inaturuhusu Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa”

Kwa uapnde wake Kamishna wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mary Longway amewataka wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kufikisha elimu ya mpiga kura kwa wananchi wao ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu.

Jaji Mst. Longway aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwa wajumbe wa mkutano huo kwenye uliofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Alisema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni ya kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi chote cha mwaka leongo ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba na kujitokeza kushiriki kuchagua viongozi wao.

“Elimu hii inawajengea wananchi ufahamu na ulelewa kuhusu haki na wajibu wao katika kushiriki katika na wawezesha wananchi na wadau wa uchaguzi kupata taarifa sahihi kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani” alisema Jaji Mst. Longway na kuongeza:

“Tunawaomba wajumbe wa mkutano huu muende mkafikishe elimu hii ya mpiga kura kwa wananchi mnaowaongoza ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu na kutekeleza haki na wajibu wao kikamilifu”

Katika mkutano huo wajumbe kutoka halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma walipata elimu ya mpiga kura na kuuliza maswali ambayo yalijibiwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa elimu ya moiga kura kupitia njia mbalimbali ili kutekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazoongoza majukumu ya Tume ambapo mbali na kutoa elimu katika mkutano huo ilitarajiwa kutoa elimu kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Sengea.



Picha zote na Hussein Makame, NEC

No comments: