Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, (katikati) na viongozi wengine kutoka kushoto,
Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (Waziri Mkuu), Waziri wa Biashara na
Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba,
wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo
cha cha
udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar
es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16,
2016
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016.
Kituo hicho kipya na cha kisasa, kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na Tanzania, chini ya mpango wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
“Serikali
ya awamu ya Tano, iliwaahidi Watanzania, wakati tukiomba kura, ya
kwamba, tutaboresha huduma ya umeme kote nchini, na leo hii ni ushahidi
tosha tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.” Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Akimkaribisha
waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo
amesema, watanzania wanahitaji umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho
ni jawabu la kuwapatia umeme ulio bora.
“Kati
ya vitu ambavyo sitarajii kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya
umeme, kuusu bei tutakaa, pembeni na watu wa TANESCO kulizungumzia
hili. “ Alitoa hakikisho Waziri Muhongo.Kwa
upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai
Mykkanen, alisema, teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho
ni ya kisasa ijulikanayo kama Distribution SCADA System, na inauwezo wa kutambua hitilafu ya umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema,
Mradi wa uboreshaji huduma za umeme jijini Dar es Salaam ulibuniwa kwa
lengo la kuboresha miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme katika sekta za kiuchumi hususan katika maeneo ya katikati ya jiji, Kariakoo, Ilala na maeneo ya wilaya ya Kinondoni.
Alisema,
utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za
umeme chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre,
ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi
(Underground Transmission Line) na kwa kutumia minara (Overhead Line) ya
msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha City
Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission
Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita 6.67.
Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita 6.67.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu, kituo hiki ambacho kinajulikana kitaalamu kama
Distribution SCADA System kitawezaesha watoa huduma wetu kufuatilia kwa
haraka zaidi pale matatizo ya umeme yanapojitokeza kwa kutumia mifumo ya
ksiasa ya kompyuta.” Alifafanua Mhandisi Mramba na kuongeza.
“Nia hasa ni kujenga vituo vingine kama hiki kwa kuanza na miji mingine mikubwa ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma.” Alisema.
Waziri Mkuu na wageni wengine wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System
Waziri Mkuu akitembeela moja ya mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server)
Mtaalam
wa mitambo, wa shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua
Turkey, kushoto, akimpatia maelezo waziri mkuu wakati akitembelea kituo
hicho muda mfupi kabla ya kukizindua rasmi
Waziri Mkuu akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akitoa hotuba yake
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen
Waziri Mkuu akipokelewa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowasili kwenye hafla hiyo
Waziri Mkuu akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Waziri Mkuu akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
Waziri Mkuu akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo
Waziri Mkuu akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba
Waziri Muhongo akizungumza na Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen
Waziri
wa Bishara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, (kushoto) na Balozi wa
Finland Nchini, Pekka Hukka, (kulia), wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo
Waziri Mkuu, akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi huo
1 comment:
Jamani nasema kwa nia njema kabisa, huu mtindo wa viongozi hata Makatibu wa Kuu kuvaa beji za majina yao kwenye shughuli yeyote ile unapaswa kuizamwa tena. wakiwa maofisini labda inafaa, sasa hata kwenye hafla nje ya ofisi? wanaonekana virojo. Hii haipo popote pale isipokuwa jeshini polisi na magereza.
Post a Comment