Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka
vijana wasisite kuleta mabadiliko chanya katika Nchi mana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa.
Ameyasema
hayo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi A mjini Kisiwani Zanziba. Amewasishi Vijana watumie baraza hilo kama tanuri ya kutengenezea mbinu za uongozi na pia kama
daraja la kuanzishia vikundi vya ujasiriamali na uzalshaji mali na kutengeneza njia mbalimbali za kuinua
uchumi na kutowafanya kuwa tegemezi.
Akijibu risala ya Vijana hao ambayo imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo la Vijana Bi Farida Juma
ambapo walitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na uhaba wa fedha, Waziri Makamba amelitaka
Baraza hilo kufungua akaunti na yeye atawapatia mchango wake wa shilingi milioni mbili.
Awali akimkaribisha Mheshimwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A, Mheshimiwa
Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na pia wahakikishe wanalinda na
kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi yetu.
Wakitoa shukrani zao kwa Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Baraza hilo la Vijana walimshukuru Mheshimiwa
Waziri kwa kuitikia wito wao wa kumuomba awe mgeni Rasmi katika siku yao hiyo adhimu.
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
akihutubia wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi ‘A’ mjini kisiwani
Zanzibar ambapo alkua Mgeni Rasmi.
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A Mh. Mwinyiusi Hassan wakati aliposhiriki
uzinduzi wa baraza la vijana la wilaya hiyo kama Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Baraza hilo .
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akionyesha cheti kama ishara
ya uzinduzi wa Baraza la Vijana wilaya ya Magharibi A.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Magharibi A, Mh Saada Mkuya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bi. Farida
Juma na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi ‘A” Mh Mwinyiusi Hassan.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia zawadi alizopatiwa
na Braza la Vijana Wilaya ya Magharibi A.
No comments:
Post a Comment