Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewaasa abiria kutoa taarifa pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao katika vyombo vya usafiri.
Masauni ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.
Amesema dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambao ndio nguvu kazi ya taifa.
Amesema kampeni hiyo iweze kuleta matokeo chanya ambayo yataonyesha kupungua kwa ajali au kutokuwepo kwa ajali na kufanya watanzania kuwa salama katika vyombo vya usafiri.
Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani.
Amesema abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.
Mjumbe Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni italeta mageuzi katika kupunguza ajali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti
ndani ya basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini
Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliandaliwa na Mabalozi wa RSA kwa
kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na abiria mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti
katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka
abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na
pia kila abiria ni wajibu wake kujua haki zake. Kushoto ni Mlezi wa RSA Taifa
ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kulia) akimsikiliza Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) Taifa,
Asina Omary alipokuwa anatoa historia ya RSA pamoja na majukumu yake kabla
ya Naibu Waziri huyo kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu
cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliratibiwa na
Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto) akienda kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti na Mabalozi wa
Usalama Barabarani nchini (RSA) ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini
Dar es Salaam. Masauni alizindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyoratibiwa na
Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Watatu kushoto
ni Mlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni akizungumza jambo katika hafla uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam.
Masauni baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani inayoratibiwa na Mabalozi wa Uslama Barabarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azani (kushoto) ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Usalama barabarani akifatilia hotuba ya mgeni rasmi hayupo pichani katika uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sumatra,Gilian Ngewe akizungumza katika kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Kamanda Kikosi cha Usalama Babarani (DCP), Mohamed Mpinga ndani ya moja ya mabasi katika kituo cha Mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha Ubungo katika uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katiika katika uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandis Hamadi Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahamasihaji wa mauala ya ualama barabarani na viongozi engine wa kamati za usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment