Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji, Charle’s Mwijage amefanya ziara kutembelea viwanda vilivyopo Mkoa wa Pwani na kuangalia maendeleo ya mkoa huo katika sekta ya viwanda.Katika ziara hiyo Waziri Mwijage alipotembelea kiwanda cha Viuadudu cha kibaha, Sayona Fruits, Global Packaging kiwanda cha kuunganisha matrekta pamoja na kiwanda cha Eveline.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwijage amesema ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani unakua kwa kasi na kuonngeza ajira kwa watanzania.
Amesema kitendo cha mmiliki wa kiwanda cha Sayona kuwapa wanakikjiji fursa ya kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu na kisha kuajiliwa katika kiwanda hicho ni uungwana ambao watafanya kazi ya kufundisha wafanyakazi wenzao.
“Wafanyakazi wa Sayona kupatiwa fursa ya kwenda chuo kikuu kujifunza ili kuja kuwafundisha wenzao, kasi hiyo imenifurahisha sana” amesema Waziri Mwijage.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili mkoani pwani kwaajili ya ziara ya siku moja.
.Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s akizungumza na meneimenti ya kiwanda cha viua vidudu kilichopo kibaha, mkoani Pwani Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwada hicho,Samwel Mziray mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda Viua Vidudu hicho,Samwel Mziray katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha viua vidudu, Kibaha.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Global Packaging, Wasonga Otieno mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akisalimia wafanyakazi wa kiwanda cha Sayona mbele mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majjid Mwanga
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa wa Pwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment