Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akiongea na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (mweyesuti) alipotembelea
chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni
hapo ikiwemo Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4,Projecta 4 na Komputa 22, wa mwisho kulia
ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent mwenye suti akiongea na
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda(mwenye shati
jeupe) ambapo alishauri kusimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano vinatumika kwa manufaa ili kuleta matokeo yenye tija, Makamu Mkuu wa Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano
wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakifuatilia maelekezo ya
namna ubao maalum wa smart board unavyofanya kazi wakati wa kufundishia ikiwa ni moja ya msaada
uliotolewa na mamlaka ya elimu.
Sehemu ya Komputa 22 zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwenye chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (katikati) akiongea na
wanafunzi wanaonufaika na msaada wa vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano vilitolewa
katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Misaada mingine iliyotolewa ni Projecta 4 na
Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa
Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda na kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Tumaini Katunzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent(kulia) akimkabidhi Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda moja ya projecta
zitakazotumika katika kufundishia chuoni hapo, Misaada mingine ni Ubao maalum za kufundishia (Smart
Board) 4 na Komputa 22,wanaoshuhudia kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe na kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Tumaini
Katunzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent(kushoto) akiwaeleza jambo
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda (katikati) na
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi (kulia)
alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
walivyovitoa chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment