Friday, November 25, 2016

VIJANA KUONESHA VIPAJI VYAO HADHARANI MASHINDANO YA ULEGA CUP MKURANGA

 Diwani wa Kata ya Panzua Bw Juma Magaila akiongea na waandishi wa habari kuhusu ligi ya Ulega Cup  inayoendelea  Wilayani Mkuranga.
Katibu wa mbunge wa mkuranga Bw Omar Kisatu Akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.
 Katibu wa mbunge wa Mkuranga Bw Omar Kisatu akipeana mikono na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki mashindano ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.
 Diwani wa Kata ya Mkamba Wilayani Mkuranga Bw Hassan Dunda Akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Mtiririko mzima wa ligi ya Ulega Cup unaondelea huko Wilayani Mkuranga.




VIJANA wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wamesema kuwa kitendo cha Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kupiga marufuku kukodi wachezaji Kutoka Nje ya Wilaya hiyo imeleta changamoto kwao kuonesha vipaji vyao Kwenye ligi ya mbunge inayoendelea.

Wamesema kuwa wao kama vijana ndio wakati muafaka kwao kuonesha vipaji vyao na uwezo ili mwisho wa siku wapate nafasi ya kushiriki Kwenye ligi mbalimbali.Mbunge Ulega ameazisha Ligi ya mbunge ambapo hivi sasa timu Kutoka kila kijiji zinapambana na baadae zitatoa timu moja ya Kata ambayo itakwenda kushindana na Kata zingine zilizopo ndani ya Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumzia ligi hiyo jana wilayani humo Kijana khatibu Dadi alisema kuwa mbunge Ulega amedhamiria kuinua vipaji vya vijana wa Mkuranga na hiyo nikutokana na wito wake wakutaka ligi hiyo ishirikishe vijana wa maeneo husika tofauti na wanavyofanya kungineko."Kwa kifupi kila mtu anampongeza Mh.Mbunge Kwa uamuzi wake kwani lazima ifike wakati sisi kama vijana wa Mkuranga tuoneshe wenyewe uwezo na vipaji vyetu na tunaamini kupitia ligi hii ya Mbunge tutapata timu kabambe ya Wilaya."alisema Dadi

Akizungumzia mwendelezo wa Ligi hiyo Katibu wa Mbunge Omar Kisatu alisema kuwa Mashindano yanaendeleo vizuri na mwitikio ni mkubwa na vijana wako kwenye morali ya hali ya juu.Alisema kuwa hatua inayoendelea sasa ni ya timu za vijiji kupambana na kuna kamati maalumu ambayo Kazi yake nikuangalia vijana wenye uwezo watakao tengeneza timu ya Kata.

Aliongeza kuwa ligi hiyo Kwa sasa ipo chini ya u simamizi wa Madiwani na ikishafika kwenye hatua ya kushindana kata Kwa Kata hapo Mbunge ataingiza nguvu zake moja Kwa moja."Kama mnavyoona ligi inaendelea vizuri na hapa katika ngazi hii Madiwani ndio wanasimamia lakini ikishafika Kwenye ngazi ya Kata na kuendelea Mh.Mbunge atakuwa ndio mfadhili mkubwa."alisema Kisatu.

Ligi hiyo imeshirikisha timu 125kutoka katika vijiji vyote 125 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na itarajiwa kupatikana timu 25 zitakazo cheza ngazi ya Kata.

No comments: