Timu ya wazungumzaji wa Fursa
wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja
na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akizungumza na vijana waliohudhuria semina ya Fursa mkoani Dodoma mwishoni
mwa wiki hii.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa
(UN) nchini, Hoyce Temu akitoa mafunzo ya
malengo ya maendeleo enedelevu kwa vijana wa Dodoma waliojitokeza wakati
wa semina za Fursa zilizofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki hii
Baadhi ya vijana waliojitokeza kwa
wingi kuhudhuria mafunzo ya Fursa mwishoni mwa wiki hii mkoani Dodoma
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na
Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na vijana
wakati akifungua semina ya Fursa iliyofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki
Mmoja wa wazungumzaji wa semina
za Fursa, Yahaya Nawanda akizungumza na vijana kwenye siku ya pili ya
mafunzo ya kilimo na ufugaji yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii mkoani
Dodoma.
Mwanzilishi wa Fursa , Ruge
Mutahaba akizungumza na vijana wakati wa siku ya pili ya semina za Fursa
zilizofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki hii
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akimkabidhi mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce
Temu.
Baadhi ya vijana waliopata
mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini
Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu
Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja
na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce
Temu.
Umoja
wa Mataifa umeingia ushirikiano na FURSA ili kuongeza uelewa wa malengo
ya maendeleo endelevu kwa vijana zaidi ya 10,000 katika mikoa mitatu ya
Dodoma, Dar es Salaam pamoja na Kigoma.
Fursa, ambayo imekuwa
ikifanyika kwa miaka mitatu iliyopita, imejikita katika kuwajengea uwezo
vijana wa kuzitambua fursa katika maeneo yao wanayoishi lakini pia
namna ya kutengeneza miradi na biashara kupitia fursa hizo.
Ushirikiano
wa Fursa na Umoja wa Mataifa utalenga kuwafikia vijana wanaohudhuria
semina za Fursa kuelewa namna Malengo ya Dunia yanavyohusiana na maisha
yao ya kila siku na wajibu wa kila kijana katika kushiriki
kuyakamilisha.
Akizungumza wakati wa kuzindua semina za Fursa
mkoani Dodoma, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema
semina za Fursa zimeweza kubadilisha maisha ya vijana wengi na hivyo
ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa katika kufikia vijana utatoa nafasi
ya vijana kuyaelewa Malengo ya Dunia.
‘Vijana wengi wana ari ya
kushiriki katika kufanikisha Malengo ya Dunia, ndio maana Umoja wa
Mataifa umeamua kushirikiana na Fursa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi
wanayafahamu malengo haya lakini pia wanashiriki katika kuyatekeleza’
alisema Alvaro.
Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Fursa, Ruge
Mutahaba amesema kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Fursa imefanikiwa
kuwafikia zaidi ya vijana milioni 5, na kuwapa mbinu na maarifa ya
kuweza kutumia fursa katika maeneo yao.
‘Tunaushukuru Umoja wa
Mataifa kwa kushirikiana na Fursa kuwafikia vijana katika mikoa ya
Dodoma, Dar es Salaam na Kigoma, ili sio tu wapate nafasi ya kupata
mafunzo ya Fursa na biashara balipia mafunzo juu ya Malengo ya Dunia’
alisema Ruge.
No comments:
Post a Comment