Tuesday, November 15, 2016

TIC YAZINDUA KITENGO CHA HUDUMA ZA MAHALA PAMOJA


Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

WIZARA ya Viwanda na Biashara na uwekezaji,imeweka wazi kuwa itaendelea kuhakikisha kwamba tasisi zote zinafanya mabadiliko ya utaratibu ili kuboresha uwazi ,tija na ufanisi hili kuweza kuboresha huduma kwa wawekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alipokuwa akizindua rasmi kitengo cha Huduma za mahala Pamoja katika kituo cha uwekezaji(TIC)

“Wawekezaji tunaowahitaji Tanzania ndio haohao wanaohitajika nchi zingine hivyo serikali itaendelea kuboresha huduma zake kuwa za uwazi ,kasi na ufanisi zaidi”amesema Waziri Mwijage.

Ameongeza serikali ya awamu ya tano ipo mstari wa mbele katika kuongeza uwazi ,uwajibikaji,kupiga vita Rushwa na kubana matumizi ya serikali  na kuweka wazi kuwa hii yote itafanikiwa kama kila tasisi itawajibika kama kituo cha uwekezaji na wadau wake katika cha huduma za mahala Pamoja.

Amemaliza kwa kusema kituo cha uwekezaji Tanzania kina mchango mkubwa sana katika uchumi hasa kwa upande kwa kuhakikisha nchi inapata wawekezaji katika sekta zote ,kusaidia kuwahudumia wawekezaji  hao kufuatana na sheria hasa katika uanzishwaji na utekelezaji wa miradi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa, Adolf Mkenda pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Profesa Lucian Msambichaka wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma za Pamoja ndani ya Kituo cha Uwekezaji nchini, zilizofanyika leo Novemba 15, 2016 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari muda mfupi baada ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma za Mahala pamoja cha TIC jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Profesa Lucian Msambichaka 
Waziri wa Viwanda na Biashara ,Charles Mwijage, akizungumza na baadhi ya watoa huduma katika Kitengo hicho mara baada ya uzinduzi wake.
Waziri wa Viwanda , Biashara na uwekezaji,Charles Mwijage , akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma za Pamoja leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha mahala pamoja cha TIC jijini Dar es salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Pendo Gondwe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha mahala pamoja cha TIC jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Viwanda na Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wa uwekezaji na watendaji kutoka TIC, leo jijini Dar es Salaam.

No comments: