Sunday, November 6, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Wananchi wa kijiji cha Ikuba katika wilaya ya Mlele hawana sehemu ya kuishi baada ya operesheni ya kuwaondoa wavamizi kuteketeza nyumba na mali zao. https://youtu.be/Ebl72n_Z4gc

SIMU.TV: Serikali imetakiwa kuchukua tahadhari mapema iwezekanavyo kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifuko katika hifadhi za taifa ili kulinda vivutio hivyo. https://youtu.be/-kbmuI9MhZY

SIMU.TV: Mamlaka ya hifadhi zaq taifa TANAPA imeshauriwa kufanya tafiti  ili kubaini chanzo cha kuwepo kwa migogoro ya mipaka kati yake na wakazi wanaozunguka hifadhi za taifa. https://youtu.be/dInm7XFI9Dc

SIMU.TV: Shirika la Rafiki social Develeopment Organization limefanikiwa kuwaokoa vijana na watoto 411 walioacha shule na kuajiriwa katika ajira hatarishi za machimbo ya madini. https://youtu.be/KjJbb2DsshU

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amekagua vituo vidogo vya polisi na kubaini kuwa havikidhi kuwahudumia wananchi. https://youtu.be/xEmt95WdhOo

SIMU.TV: Wakulima wa zao la pamba katika mkoa wa Tabora wamepewa siku saba kuhakikisha kuwa wameandaa mashamba yao kulingana na maelekezo ya maafisa kilimo. https://youtu.be/R893iCe048g

SIMU.TV: Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Tanzania Building Work amempongeza rais Magufuli kwa juhudi zake za kutaka watanzania wajikomboe kiuchumi. https://youtu.be/2o7lhSESJRw

SIMU.TV: Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imekutana na wafanyabiashara wenye asili ya Asia ili kujadili namna ya kutatua kero zinazowakabili. https://youtu.be/09WAslsTbu8

SIMU.TV: Wakala wa vipimo nchini katika mkoa wa Mtwara umebaini kuwa mizani ya ghala ya TANEKU ulikua ukiwapunja wakulima wa Korosho na kuamuru urekebishwe mara moja. https://youtu.be/54UNvci67lg

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Magomeni wilayani Bagamoyo wanakaribia kuondokana na adha ya huduma ya maji baada ya kupatiwa msaada wa Kisima chenye thamani ya shilingi milioni 21. https://youtu.be/tE4hZhlzcOg

SIMU.TV: Vinara wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Simba imekubali kuvutwa shati na timu ya African Lyon kwa kufungwa bao moja kwa bila. https://youtu.be/G9NmYJdVNQU

SIMU.TV: Timu ya madiwani wa halmashauri ya jiji la Mbeya leo imeingia mitini kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya waandishi wa habari jijini humo nakufanya mchezo huo kutofanyika. https://youtu.be/Ek80Pfto184

SIMU.TV: Timu ya Arsenal imepunguza kasi ya kufukuzia ubingwa wa ligi kuu Uingereza baada ya kukubali sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Tottenham Hotspur leo. https://youtu.be/Xf8n2syiStQ

SIMU.TV: Watu zaidi ya 700 wamepoteza makazi yao baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kubomoa makazi yao huko wilayani Ukerewe mkoani Mwanza; https://youtu.be/JTKEl1trtA4

SIMU.TV: Uongozi wa mkoa wa Tabora umesema utawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi wa wilaya watakaoshindwa kusimamia utunzaji wa misitu; https://youtu.be/izhPqBYCFEU

SIMU.TV: Hifadhi ya taifa ya Kitulo imetakiwa kuhakikisha inamaliza mgogoro wa eneo hilo ili kuweza kupunguza tatizo la uchomaji moto hifadhi hiyo; https://youtu.be/zclFG5R0Xl4

SIMU.TV: Wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara, wamepongeza juhudi za serikali kwa kuboresha bei ya zao hilo kufikia kiasi cha shilingi 3000 kwa kilo; https://youtu.be/Ym1gwLhv1C0

SIMU.TV: Waziri wa Tamisemi George Simbachawene, amesema serikali inaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za maendeleo kwa wananchi; https://youtu.be/Gb3CHwoXJYE

SIMU.TV: Hospitali ya taifa ya Muhimbili imezindua huduma maalumu ya kuwapatia tiba watoto wenye matatizo ya kusikia vizuri kwa kuwawekea vifaa vya kusikia; https://youtu.be/8h4N-6kOvCw

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu; https://youtu.be/ScVNN39aUNA  

SIMU.TV: Timu ya soka ya Yanga imeamsha matumaini ya kutetea taji lake la ligi kuu baada ya hii leo kuchomoza na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons; https://youtu.be/1caZbq78hks

SIMU.TV: Mashindano ya netiboli kombe la Muungano, yameanza kutimua vumbi lake katika viwanja vya Sigara huku timu za Zanzibar zikianza kwa kupoteza michezo yake; https://youtu.be/7mWTJaFayzM

SIMU.TV: Timu ya Pan African yenye makao makuu yake jijini Dar Es salaam imefanya uchaguzi wake mkuu na hii hapa ndio orodha ya viongozi wake wapya; https://youtu.be/Y3yL40ZCEs8

SIMU.TV: Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena hii leo kwa kupigwa michezo mbalimbali, huu hapa mkusanyiko wa matokeo kwa mechi zote; https://youtu.be/JDUSteKjhwM


No comments: