Sunday, November 6, 2016

SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WAPONGEZWA KWA KUWA NA UBUNIFU

SHIRIKISHO la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu wamepongezwa kwa hatua ya kuanzisha jukwaa linalowakutanisha baina yao na viongozi wa Chama na Serikali ili kupata fursa ya kufahamu kinachoendelea na kutoa ushauri. 
Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi Kirumbe Ng’enda alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kutathmini siku 365 za uongozi wa Mhe. Raios Dkt. John Pombe Magufuli katika Sekta ya elimu. 
Ng’enda amesema kuwa mbinu hiyo ya kuwaita na kukaa nao pamoja viongozi wa kiasiasa na Serikali kutasaidia sana kwa makada wa Chama kujua shughuli mbalimbali za maendeleo nhivyo kuwaweka katika hali nzuri ya kujibu mashambulizi pindi yanapojitokeza. 
“Ni likuwa naongea na Katibu wenu Zenda ameniambia kuwa huu utaratibu wa kukutana na viongozi utakuwa endelevu, ni vyema ni waambie tu hatua hiyo ni muhimu sana na sina budi kuwapongeza kwa ubunifu huo.”Alisema Ng’enda. 
Naye Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo amesema kuwa wao kamashirikisho wamejipanga vyakutosha kuahakikisha sasa wanakuwa mstari wa mbele kukisaidia chama na Serikali kwa rasilimali watu ipo ya kutosha kufanikisha azma hiyo. 
Alitumia wasaa huo kuwaomba wanachama wote wa Shirikisho hilo nchini kuwa karibu na wanafunzi wenzxao na kushirikiana nao katika shida na raha kwani kwa kufanya hivyo ndiyo utendaji unaotakiwa katika awamu hii ya Mhe. John Pombe Magufuli. 
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Daniel Zenda alisema kuwa wao kama Shirikisho ni wajibu wao wa kukishauri Chama cha ili kuleta matokeo chanya na kuongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kufanya tathmini ya namna Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilivyotekeleza ahadi yake katika sekta ya Elimu ndani ya mwaka mmoja. 
Aidha Zenda alitumia fursa hiyo pia kumpa pongezi Rais John Magufuli kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kwa kusikiliza kilio cha wanafunzi hali hiliyopelekea kurekebisha baadhi ya vigezo kwa waombaji wa mikopo. 
Zenda amesema kuwa inatia faraja kuona siku moja baada ya Shirikisho kutoa tamko kuhusu masula mbalimbali yanayohusu mikopo ya elimu ya juu, Waziri mwenye dhama alichukua hatua ambazo kimsingi zimeonyesha ni namna gani Serikali yetu ilivyo sikivu. 
“Kwa dhati kabisa naipongeza Serikali ya Rais Magufuli kwani imeonyesha usikivu wa hali ya juu,lakini pia kipekee nimpongeze mama yetu Mhe. Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako kiukweli ameonyesha kuwa ni kiongozi anayejali wanyonge”. Alisema Zenda. 
Shirikisho hilo limeanzisha Jukwaa litakalo kuwa linawakutanisha wadau pamoja na kujadiliana masuala mbali mbali ya kitaifa ambapo mwishoni mwa mwezi novemba limepanga kujadili azma ya Serikali kuwa na Tanzania ya Viwanda.






 Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Utawala ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Kirumbe Ng’enda akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu wa Chama hicho(hawapo pichani) wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina na Katibu Msaidizi wa Shirikisho Bw. Daniel Zenda.
 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina akizungumza jambo katika wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ambaye pia kwa sasa anashikiria nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Daniel Zenda akifafanua jambo wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Taifa, Bw.Hamid Saleh Mhina
 Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ambaye pia ndiye alikuwa Mratibu wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ndugu Mgwanwa Nzota akielezea jambo wakati wa Kongamano hilo jana Jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula akizungumza wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Taifa, Daniel Zenda, mgeni rasmi katika kongamano hilo ambaye pia ni mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (Mnec) Kirumbe Ng’enda na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Taifa, Hamid Saleh Mhina.
 Mgeni rasmi katika Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bw. Kirumbe Ng’enda akiteta jambo na Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania Bw. Daniel Zenda (kulia) wakati wa kongamano hilo jana Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Taifa, Bi. Deborah Charles, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Mgeni rasmi (Mnec) Kirumbe Ng’emba wakiandika hoja zilizoibuliwa na washiriki wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli lililofanyika Jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wanachama wa Shirikisho hilo kutoka vyuo mbalimbali vya Jijini Dar es Salaam baada ya Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli  kumalizika jana Jijini Dar es Salaam.

No comments: