Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),
Bi. Eda Sanga na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka
asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama
barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka
Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),
Bi. Eda Sanga (katikati) na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa
wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera
ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa
Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba
20, 2016. Kulia ni Jones John kutoka Taasisi ya Jukwaa la Haki za
Watoto Tanzania na Mwakilishi kutoka TAWLA, Nasieku Kisamby (kushoto).
Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John (katikati)
akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za
Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za
TAMWA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Gladness Munuo kutoka TAMWA
MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA. SIKU YA KIMATAIFA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI 20 NOVEMBA, 2016.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Matukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.
Takwimu
zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila
mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50
hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani
(WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi zimetokea
Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.
Takwimu
pia zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwa sababu ya makosa ya
kibinadamu hasa uzembe wa madereva kutokutii sheria na kanuni za
barabarani, ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi nchini
Tanzania, asilimia 76% ya ajali barabarani husababishwa na uzembe wa
madereva, asilimia 8% husababishwa na ubovu wa barabara. Aidha ubovu wa
vyombo vya moto husababisha ajali kwa asilimia 16%.
Hata
hivyo ajali nyingi zinaepukika kama madereva na watumiaji wengine wa
barabara watazitii sheria na kanuni za Usalama barabarani. Kutokana na
ajali hizo kuongezeka ndio maana ikatengwa siku maalum ya kimataifa ya
kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani kila mwaka ambayo
huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Novemba ya kila mwaka. Siku hii
inatambulika kama siku rasmi ya kimataifa ya kuwakumbuka waathrika wa
ajali hizo na familia zao na kuzitaka nchi wanachama pamoja na jumuiya
za kimataifa kuitambua siku hiyo.
Pia
siku hiyo hutoa fursa kwa jamii nzima kukutana na kuwakumbuka wahanga
wa ajali za barabarani ,kutafakari madhara, gharama, na hatua zinazoweza
kuchukuliwa katika kuzuia ajali zisitokee. Vilevile siku ya kuwakumbuka
wahanga wa ajali za barabarani inatoa nafasi kwa wadau kuikumbusha
serikali wajibu wake na jamii nzima katika suala la kuzifanya barabara
kuwa sehemu salama kwa kila mmoja.
Hivyo
basi mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya
sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania kama ambavyo
unaratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria (TAWLA) pamoja na mambo
mengine katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria
kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili
iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na
athari zinazotokana na ajali hizo Maeneo ndani ya sheria ambayo mtandao
huu utajielekeza kuona sheria inafanyiwa mabadiliko/maboresho ni pamoja
na;
Matumizi
ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa
kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda
wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria
wanaokaa kiti cha nyuma.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu. Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu. Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.
Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemii chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho.
Vilevile pamoja na kuanishisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutovaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa. Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa na kwa usahihi.
Hivyo
basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika
kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo
ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda
pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.
Matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili.
Kiwango
hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika
la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva
aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga
(young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho
ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.
Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisiszokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.
Tunatoa wito kwa watunga sera kutaka kujihulisha zaidi na wadu kuuelimisha umma zaidi katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo. Mwakilishi kutoka Chama cha wake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Nasieku Kisamby (wa kwanza kushoto) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kutoka kulia ni Gladness Munuo, Jones John na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga. Ofisa Mradi Msaidizi kutoka Tanganyika Law Society (TLS), Mabhezya Rehani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Meza kuu ikiwa imesimama kwa dakika mbili kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na ajali katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Christina Thomas mkazi wa Kibaha na mmoja wa waathiriwa wa ajali za barabarani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Salum Juma Haji (kulia) makazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam akizungumza jambo katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Mkutano kati ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo ukiendelea.
No comments:
Post a Comment