Friday, November 25, 2016

MASAUNI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA YA POLISI JIJINI DAR LEO, AWATAKA WATEKELEZE MAJUKUMU YAO KWA VITENDO

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (aliyevaa tai) kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (wapili kulia), Kamishna wa Fedha wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Merise Mwanyema wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Naibu Waziri kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza ipasavyo maazimio ya kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia meza kuu) kufungua Kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi kutoka Zanzibar, Shemsa Said akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Masauni aliwaambia waandishi hao, Jeshi la Polisi linaendelea kupambana na madawa ya kulevya pamoja na kulinda usalama wa raia na mali zao nchini ikiwa ni sehemu ya majukumu yao. Pia aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza ipasavyo maazimio yote ya kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: