Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akifungua mafunzo hayo kwa Watumishi
wa TPA na TRA yanayohusu matumizi ya ‘scanner’ mpya iliyofungwa katika
Bandari ya Dar es Salaam.
Baadhi
ya Watumishi wa TPA ambao watahusika na usimamizi wa matumizi ya
‘scanner’ mpya wakati wa ukaguzi wa mizigo ya kontena katika Bandari ya
Dar es Salaam.
Afisa
Forodha Mwandamizi wa TRA, Bw. Julius Joseph akichangia jambo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo alitoa rai kwa TPA na TRA kuendelea
kushirikiana kwa pamoja wakati wa ukaguzi wa mizigo katika Bandari za
Tanzania ili kuondoa mianya ya ukwepaji kodi na kuongeza mapato ya
Serikali.
Afisa
Ufundi anayehusika na scanner kutoka TRA, Bw. Manjale Musele akichangia
jambo kuhusiana na namna walivyojipanga katika kuhakikisha ‘scanner’
mpya inatumika kikamilifu ili kuisaidia Serikali kuongeza mapato.
Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akisisitiza jambo kwa washiriki wa
mafunzo ambapo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wakati watakapokuwa
wanaendesha scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Fredy Liundi,
Kaimu Mkurugenzi wa Utumishi, Bw. Erasmo Mbilinyi na Kaimu Mkurugenzi wa
Tehama, Bw. Abdulrahman Mbamba (kulia).
Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Eng. Deudedit Kakoko akifurahia jambo na Meneja Mafunzo
kutoka Kampuni ya Nuctech ya Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Lan Yuming
mara baada ya kuzindua mafunzo kwa Maafisa wa TPA na TRA hivi karibuni.
Katikati ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Nuctech Bw. Zhang Sheng.
Jengo jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya matumizi ya scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment