Friday, November 4, 2016

ISRAEL YAZINDUA KITUO CHA VIZA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (Mb) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe za kufungua Kituo cha Kutoa viza za kwenda nchini Israel akiwasilisha hotuba katika ufunguzi huo. Prof. Maghembe alipongeza uamuzi wa Israel kufungua kituo hicho hapa nchini kwa kuwa kitarahisisha ziara za kwenda Israel kwa Watanzania. Aidha, alirejea kauli ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu dhamira ya Serikali ya kufungua Ubalozi nchini Israel. 


Prof. Maghembe alieleza kuwa idadi ya watalii kutoka Israel kuja Tanzania inaendelea kuongezeka na jana alikutana na wakala wa usafirishaji kutoka nchi hiyo ambao wana nia ya kuanza safari za ndege za kila wiki kutoka Israel hadi mkoani Katavi (charter flights) kutembelea maoeneo ya utalii. Ndege aina kama hiyo inafanya safari za kuja Tanzania katika mikoa ya kaskazini mara mbili kwa mwaka. Prof. Maghembe alisisitiza umuhimu wa Tanzania kushirikiana na Israel katika sekta ya teknolojia hususan mbinu za kitaalamu za kukabiliana na ujangili wa wanayamapori nchini.Kituo cha viza kitakuwa na ofisi za muda kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Israel nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Yahel Vilan akitoa neno la ukaribisho wakati wa sherehe za ufunguzi. Alisema anashukuru Mungu ametimiza ombi alilotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana naye Ikuku, Dar es Salaam. Mhe. Rais aliomba Serikali ya Israel ifungue Kituo cha Viza hapa nchini jambo ambalo limetia leo hii. Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi maarufu nchini Israel, hivyo anatarajia ahadi ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini humo litatekelezwa hivi karibuni. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima (kushoto) akifuatilia hotuba za sherehe za ufunguzi wa kituo cha viza cha Israel .
Balozi wa Israel akihutubia washiriki wa sherehe za ufunguzi wa kituo cha viza. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Yahel Vilan wakikata utepe kuashiria kituo cha kutoa viza cha Israel kimefunguliwa rasmi. 
Ofisi ya Kituo cha Kutoa Viza cha Israel ambacho kwa sasa kipo katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 
Picha ya pamoja. 

No comments: