Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam,
Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria
kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), wakikata utepe kuzindua
rasmi Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ wakati wa hafla ya uzinduzi huo
uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jacckline
Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi
ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally.
Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar
es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada
wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), na Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) Mkaguzi
wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni (kushoto) na Jackline
Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam, kwa pamoja wakiinua vipeperushi baada
ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ iliyofanyika
kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog
Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Sehemu ya wadau na mashuhuda waliohudhuria uzinduzi huo.
Specioza Sylvester, mkazi wa jijini Mwanza akitoa ushuhuda wa Ukatili jinsi alivyomwagiwa Tindikali na vijana waliotumwa na mumewe kwa ajili ya mali.
Rukia Hamis, mkazi wa Mbagala Kijichi, akitoa ushuhuda jinsi alivyokatwa mkono na mumewe.
Rukia akiuvaa mkono wake wa bandia baaada ya kutoa ushuhuda
Jacckline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia kutoka Shirika la Oxfam, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la
Jinsia Polisi Kinondoni, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, akizungumza.
Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue, akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wadau na viongozi wakiwa Jukwaa Kuu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwacity
Almas, akiimba na kucheza pamoja na baadhi ya kinamama waliohudhuria uzinduzi
wa Awamu ya tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ ya Kituo cha Msaada wa Sheria kwa
Wanawake (WLAC), iliyozinduliwa leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Kinondoni,
jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Hisia Theatre Group, wakitoa burudani.
Wasanii wa kikundi cha Ngonjela cha Aha Organization, wakighani mashahiri yao ya Ngonjela.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Hisia Theatre Group, wakitoa burudani.
No comments:
Post a Comment