Picha ya pamoja ya wasichana 14 waliojitolea kufanya kazi ya kufyatua matofali kusaidia ujenzi wa mabeni na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Nasibugani. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Felbeto Sanga wa kulia,akizungumza na baadhi ya wadada walijitolea kufanya kazi hiyo. |
baadhi ya matofali yaliyo fyatuliwa na vijana hao waliojitolea |
Moja ya chumba kinachotumiwa na wanafunzi hao kulala kwa kuweke magodoro chini. |
Moja ya Bweni linalotumiwa na wanafunzi shuleni hapo linavavyoonekana.
Mwezi mmoja uliopita vijana wazalendo walitembelea Shule ya Sekondari ya Nasibugani umbali wa KM 98 toka Dar es salaam,iliyoko Mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga kwa wito wa Mkuu wa wilaya hiyo Filbeto Sanga,ikiwa na umbali wa KM 53 vijijini ndani kutoka makao makuu ya wilaya hiyo kujionea kile kinacho wasibu Wadogo zao wasomi walioko shuleni hapo.
Walikuta chumba kimoja chenye vitanda viwili vya upana wa futi 2,2 wanalala Wanafunzi wawili wawili,chumba kimoja cha wastani chumba kilichokuwa Maabara wanalala watoto tena magodoro yakiwa chini wanafunzi 70,walikuta nyumba moja ya Waalimu yenye vyumba vitatu wanaishi waalimu 7
Tangu wiki hiyo ya tarehe 27/9/2016 hadi unasoma ujumbe huu,Wadada hawa Wazalendo na wasomi hawakurudi nyumbani,wanaikataa hali hiyo kwa vitendo kama suluhisho pekee la matatizo makubwa ya makaazi na mabweni ya Shule nyingi hapa nchini,wanashiriki kwa kujitolea ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za waalimu zitakazo kidhi upungufu katika Shule hiyo.
Hamasa hii imewapa changamoto kubwa vijana wa kiume 39 walioamua kuungana na Wakinadada 14 hadi unasoma uzi huu Tayari wamekwisha fyatua Matofali 45,000 yanayokidhi Mabweni matano na nyumba tano za Waaalimu
Vijana hao wanakula chakula kile kile wanachokula wanafunzi hawo,na kuisha mazingira kama wanafunzi,
Serikali Mkoani Pwani inasema haijawahi kutokea kwa Miongo mingi ya Umri wa Taifa hili:
Akizungumza mmoja wa kijana aliyejitolea Happines Komba amesema kuwa ameamua kujitolea kufanya kazi ili kusaidia shule hiyo kupata majengo yatakayo wawezesha wanafunzi kuishi katika mazingira mazuri.
“nimepata nafasi ya kusoma na kumaliza chuo nikaona nina kila sababu ya kutumia nguvu zangu kusaidia kazi za jamii nimesukumwa na uzalendo kuja huku kufanya hiki kwa ajili ya taifa”alisema Bi Komba
Ameongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kulitumikia taifa na kuacha kuchangua kazi kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo ya taifa,na kuongeza kuwa vijana kuamka na kufanya kazi.
“mimi ni dada nina shahada kutoka chuo cha IFM nipo huku tunafyatua matofali na kwa siku tunafyatua matofali mpaka 2000 kwa siku kwahiyo wadada wasijiweke nyuma”alisema Komba
Kwa upande wake Rosemunda Mgimba aliyemaliza chuo kikuu cha dare s salaam na kupata shahada ya sayansi ya siasa,alisema kuwa amejitoloea baada kusikia taarifa ya shule hiyo wanafunzi kulala kwa shida kutokana na kukosa mabeni ya kutosha.
“niliumia sana kusikia wadogo zetu wanapata shida ya kulala na wako shule nikaona nina uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya nchi yangu na ndio sababu nipo huku kusaidia kutatua tatizo sikutaka kuwa sehemu ya kulalamika bali kutenda.’alisema Rosemunda
Aidha aliongeza kuwa vijana wawe na moyo wa kujitolewa kwa kuangalia matatizo ya nchi na kuwakumbusha kuwa wanawajibu wa kulitumikia taifa kwa ajili ya faida ya wengine na kutumia muda wao kutatua changamoto zilizopo zinazohitaji nguvu kazi.
Naye Petro Magoti amesema kuwa wameguswa na kuamua kuweka kambi katika shule hiyo ili kusaidia kumaliza tatizo hilo kwa kutumia nguvu kazi inayoshirikisha vijana 53 huku 14 wakiwa ni wanawake.
“kwa kweli mambo yamebadilika sana ukiangalia hapa kuna wadada 14 ambao tumekaa nao huku kufanya kazi hii ya kufyatua matofali na wanafanya kazi kubwa sana kusaidia taifa letu”alisema Magoti
Magoti amesema kuwa shule hiyo imezidiwa na wingi wa wanafunzi na kuamua kutumia nguvu kazi katika kusaidia serikali kutatua changamoto hiyo,na kuongeza kuwa wamefyatua matofali zaidi ya elfu 45,000 kwa ajili ya ujenzi huo.
“imefika wakati vijana kujiuliza wanataka kufanyia nini taifa lao na sio taifa limewafanyia nini” alisema Magoti
Kwa upande wake Lulu Kamaramo aliyesoma chuo kikuu nchini Malysia aliesema kuwa uzalendo ndio kitu muhimu katika nchi kwani ndio uliomfanya kufanya kazi hiyo bila kujali elimu aliyokuwa nayo.
“vijana tujifunze uzalendo ili kusaidia seriikali kwani Rais wetu anajitahidi kufanya kazi ya kutuletea maendeleo tuna kila sababu ya kufanya kazi hizi kwa kutumia muda wetu na nguvu tulizonazo”alisema Lulu
No comments:
Post a Comment