Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza Makamu Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula mara baada ya
kuwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la
Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo
Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere(MNMA).Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack
Mwakalila, Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Jamhuri msaafu Mhe. Anne Makinda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku akiwasilisha mada kuhusu Miiko ya
Uongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu
Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo
yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl.
Nyerere afariki dunia.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula akiwasilisha mada kuhusu
Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za
Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo
yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl.
Nyerere afariki dunia.
Balozi mstaafu Ibrahim Kaduma
akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la
Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo
Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka
17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano
la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakifuatilia mada
kutoka kwa wawasilishaji ambao ni Mhe. Phillip Mangula, Joseph Butiku,
Ibrahim Kaduma na Dkt. Harun Kondo, mada zilizowasilisha ni pamoja na
Miiko ya Uongozi, Azimio la Arusha na Maadili ya Viongozi.
Mchumi Mwandamizi Profesa Ibrahim
Lipumba akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi
za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho
hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa
Mwl. Nyerere afariki dunia.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha Stella Marios cha Mtwara Padre, Dkt. Charles Kitima akichangia mada
wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius
Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa
ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki
dunia.
Watoa mada wakinukuu michango ya
washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius
Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa
ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki
dunia.Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM – Bara, Mhe Phillip
Mangula, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph
Butiku, Balozi mstaafu Ibrahim Kaduma na Mwanasiasa Mkongwe Mhe. Wilson
Mkama.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano
la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakiangalia baadhi
ya maandiko na machapisho aliyoandika Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere enzi za uhai wake yanayochapishwa na Mkuki na Nyota Publisher leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za
Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo
yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl.
Nyerere afariki dunia.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiteta jambo na mmoja wa
washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius
Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA).Naibu Waziri huyo ndiye alikuwa
mgeni rasmi katika Kongamano hilo. Lililokuwa limebeba nukuu ya Mwalimu
Nyerere isemayo “Viongozi ni lazima wawe mfano mzuri kwa wananchi kwa
maisha yao na vitendo vyao pia”.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kongamano la
Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo
Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere(MNMA) akiagana na washiriki.
Picha na. Frank Shija, MAELEZO.
No comments:
Post a Comment