Wawekezaji wa AMC Ltd na viongozi kutoka halmashauri wakisoma ramani ya eneo la shamba la mkonge la kwamgwe.
Mkurugenzi mtendaji Bw. William Makufwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya bondo na majanini kata ya kwamgwe.
Mkuu
wa wilaya ya halmashauri ya wilaya ya handeni Mh. Godwin Gondwe
akizungumza na wananchi wa vijiji vya bondo na majanini kata ya kwamgwe
Mwanasheria
wa halmashauri ya wilaya ya handeni Bw. Mangesho akiwaeleza wananchi
kuwa kukaa muda mrefu sehemu haimaniishi ndio mtu anakua navumiliki
halali wa eneo.
Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wakijitambulisha kwa wananchi wa vijiji vya bondo na majan
Mh. Sharifa Abebe diwani wa kata ya kwamgwe akishukuru uongozi wa halmadhauri, wawekezaji na wananchi kwa kufikia muafaka.
Baadhi ya wananchi wa vijiji vya bondo na majanini na walioketi viti vya mbele ndio viongozi wa kampuni ya AMC ltd.
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akiambatana na kamati ya ulinzi
na usalama na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri pamoja na wawekezaji
wa shamba la mkonge la Kwamgwe Kampuni ya AMC LTD wamefanya ziara na
kuongea na wananchi wa Vjiji vya Bondo na Majanini namna ya kuachia
maeneo ambayo wananchi hao wamevamia katika shamba hilo kwa kufanya
makazi na kulima mazao ya kudumu hali iliyopelekea muwekezaji huyo
kushindwa kuendelea na shughuli zake.
Akizungumza
na wananchi mwakilishi wa Mkurugenzi bodi ya mkonge Bw.Fredrick
Sospeter alisema shamba hilo ni mali ya kampuni ya AMC LTD ambayo
walinunua toka 2002 baaada ya CRDB BANK kutangaza kuuza eneo hilo kwa
kile kilichodaiwa kuwa mwekezaji wa awali aliyejulikana kwa jina la
CHAVDA kushindwa kurejesha fedha za mkopo alizokuwa akidaiwa na hivyo
kuamua kuliuza shamba hilo ili kufidia deni alilokua akidaiwa.
BW.
Fredrick alisema kuwa awali serikali ilipanga kutoa ekari 500 kwa
wanachi waliovamia ili wapate eneo la kulima na kuacha eneo la mwekezaji
wazi ili kuruhusu shughuli za mwekezaji kuendelea. Dhamana hiyo
imechukuliwa na mwekezaji AMC kugawa ekari 500 ambapo ekari 200
zitagawiwa kwa wananchi wa kijiji cha Bondo na ekari 300kijiji cha
majanini. Ilielezwa kuwa watakao gaiwa watakuwa ni wale waliovamia na
kukaa kwa muda mrefu. Mgao huo utakua pembezoni mwa Kijiji ambapo
kimeishia na kwamba maeneo ya kulima yatakua ndani ya Kijiji husika.
Wananchi
wanaolima mazao ya kudumu utaratibu utawekwa ili kuwawezesha wananchi
hao kuvuna mazao yao na hatimaye kutoa mazao yao shambani humo, aidha
wananchi ambao wanadai viinua mgongo vyao serikali inapanga utaratibu wa
namna ya kuwalipa.
Mkuu
wa wilaya Mh. Godwin Gondwe aliwaeleza wananchi kuwa watu watakaopewa
ardhi hiyo wanafahamika kwani orodha yao ilikwisha andaliwasiku za
nyuma. Pia aliwawaondoa wasiwasi wananchi kwamba shule, nyumba za ibada
na zahanati ambazo tayari wamezijenga zitaendelea kutumika bila
kuharibiwa kwa namna yoyote ile.
Wananchi
ambao wanaishi kwenye nyumba za mkonge wataendelea kuishi pia ila
wasijenge nyingine, aliwaonya viongozi au mwanachi yeyote ambaye
atathubutu kuuza eneo ambalo mwekezaji atalitoa kwaajili ya kilimo kwa
wakazi wa vijiji hivyo atachukuliwa hatua za kisheria maramoja kwani
serikali ya awamu ya tano inasimamia sheria na haki kwa kila mtu na
hivyo wasiwe na wazo la kuuza eneo lolote.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri Bw. William Makufwe aliwaeleza wananchi kwamba
wamekuja kutoa ufafanuzi wa kisheria juu ya umiliki halali wa shamba
hilo. Aliwaeleza kuwa wawekezaji wanakuja kufanya maendeleo katika
maeneo yetu hivyo tuwape muda wafanye kazi. Aidha aliwataka wawekezaji
hao kupeleka mpango kazi wa shamba hilo ili waweze kujua kama eneo
wanaweza kuliendeleza au hawawezi ili hatua stahiki za kisheria ziweze
kutekelezwa ikiwa kampuni itashindwa kuliendeleza shamba hilo kwa mujibu
wa makubaliano.
Diwani
wa Kata ya Kwamgwe Mhe. Sharifa Abebe aliwashukuru viongozi na
wawekezaji, nakuwaomba waainishiwe hizo ekari ili waanze kufanya kazi
maramoja,wameomba wawekezaji watakavyoanza kufanya kazi kipaumbele
katika ajira kiwekwe kwa wakazi wa maeneo hayo.
Uongozi
wa kampuni ya AMC LTD uliwataka waliolima mazao ya michungwa na mazao
mengine ya kudumu kuandika barua hadi kufikia tarehe 25/10/2016 kwa
mwekezaji wakitaja majina yao, mazao wanayolima, wanaomba mazao yao
yakae kwa kipindi gani hadi watakapoyavuna yote. Watendaji wametakiwa
kukaa ofisini kuanzia saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu kuwasaidia
wananchi namna ya kuandaa barua hizo.
Alda P Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
18 Octoba 2016.
No comments:
Post a Comment