Mkazi
wa Dar es Salaam Bw. Michael Francis baada ya kuhukumiwa kifungo cha
miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la
udanganyifu katika huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mshitakiwa wa Pili na wa Tatu wakiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa hatiani na kuhumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Mshitakiwa Bw. Francis muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya udanganyifu.
Mshitakiwa
Bw. Godfrey Nyika ambaye ndiye kitambulisho chake cha matibabu
kilitumiwa isivyo halali na BW. Francis baada ya hukumu.
…………………………………………………………
Na Grace Michael
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni imewahukumu wakazi wawili wa Mkoa
wa Dar es Salaam kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi
Milioni moja kwa makosa ya kujipatia huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya kwa njia za udanganyifu.
Hukumu
hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Bweguge
Obadia ambaye alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa
mashitaka umeithibitishia mahakama pasipo shaka ya aina yoyote kuwa
washitakiwa hao walitenda makosa hayo.
Waliohukumiwa
kifungo hicho ni pamoja na Bw. Michael Francis na Bw. Godfrey Nyika
ambao ni washitakiwa wa pili na wa tatu huku mshitakiwa wa kwanza Bw.
Rashid Kidumule akiaachiwa huru baada ya kuthibitika kutotenda kosa
hilo.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Bw. Obadia alisema kuwa hakuna
shaka yoyote juu ya washitakiwa hao kutenda makosa ya kujiwakilisha
katika duka la dawa la Nakiete kwa lengo la kujipatia huduma ya dawa kwa
kutumia kitambulisho cha matibabu cha mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw.
Nyika.
“Ushahidi
wa mashahidi wa mashitaka unathibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa
mshitakiwa wa pili Bw. Francis alijiwakilisha dukani kwa lengo la kupata
dawa kwa kutumia kadi isiyo yakwake na hakuna shaka kuwa mshitakiwa wa
tatu ambaye ndiye mwenye kadi alimpatia kadi hiyo mshitakiwa wa pili
hivyo kwa ushahidi huu Mahakama inawatia hatiani,”anasema Hakimu Mkazi
Bw. Obadia.
Alisema
kuwa Mahakama hiyo imezingatia makosa waliyoshitakiwa nayo washitakiwa
hao pamoja na uhusika wao katika kutenda makosa hayo. Kutokana na hali
hiyo, Mahakama ilimhukumu Bw. Francis kifungo cha miaka miwili jela au
faini ya shilingi milioni moja huku mshitakiwa Bw. Nyika akihukumiwa
kifungo cha mwaka mmoja au faini ya shilingi laki tano.
Washitakiwa
hao walitenda makosa hayo ya kujiwakilisha kwa lengo la kujipatia
huduma mwaka 2014 ambapo kesi hiyo imehitishwa kwa wao kukutwa na hatia
na kuhukumiwa adhabu hiyo.
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya afya umekuwa ukitahadharisha wanachama wake juu ya
matumizi ya vitambulisho vyao vya matibabu kwa kuonya kufanya
udanganyifu wa aina yoyote kwenye huduma zake.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari hizi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amesema Mfuko utaendelea kuchukua hatua
stahili kwa wanachama wasio waaminifu ambao watajihusisha na udanganyifu
wa aina yoyote.
“Nitoe
tu tahadhari kwa wanachama na watoa huduma wote kuwa kila mmoja ana
wajibu wa kuulinda Mfuko kwa kuhakikisha huduma anayoitoa au kuipata iko
katika njia sahihi, Mfuko hautakuwa tayari kufumba macho kwa
wanaojihusisha na udanganyifu au kuhujumu Mfuko kwa namna yoyote,”
alisema Bw. Konga.
No comments:
Post a Comment