WAKATI
Umoja wa Mataifa (UN) ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake,
imeahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya
maendeleo.
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," amesema.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiwasili kwenye viwanja
vya Karimjee akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwenye sherehe ya
kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya
umoja huo ambapo kila mwaka Oktoba 24 huadhimishwa.(Picha na Zainul
Mzige wa Modewjiblog)
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu ya umoja huo na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.
Aidha, Rodriguez amesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linasababisha umasikini kwa kuwa nguvu kazi hiyo inashindwa kuwajibika katika kuliletea taifa maendeleo.
"Ongezeko la vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto kubwa nchiniTanzania, tunahitaji kuhakikisha kwamba vijana wanawajibika katika kujiendeleza ili kupata maendeleo chanya katika maisha yao, ili kufanikisha hayo vijana wanatakiwa kuwa na ufahamu na taaluma katika kuwezesha mabadiliko ya uchumi nchini Tanzania," alisema Rodriguez na kuongeza: "Vijana wasisahau kuwa wao ni chachu ya amani na maendeleo na UN tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha vijana wanakuwa wadau wa taratibu na kanuni zilizosababisha kuundwa umoja huu, wakijua na kutambua malengo ya dunia," amesema.
Rodriguez amesema UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo nchini.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitambuliswa kwa Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini Afisa utawala na fedha, Spencer Bokosha (wa pili kulia) na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika sherehe za maadhimisho ya
miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa zilizofanyika katika
viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
"UN itashirikiana na serikali ya Tanzania kuleta maendeleo ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii," amesema.
Kwa upande wa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema serikali inatambua mchango wa umoja huo katika kuleta maendeleo nchini na kwamba itaendelea kushirikiana na umoja huo.
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," amesema.
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu ya umoja huo na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.
Aidha, Rodriguez amesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linasababisha umasikini kwa kuwa nguvu kazi hiyo inashindwa kuwajibika katika kuliletea taifa maendeleo.
"Ongezeko la vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto kubwa nchiniTanzania, tunahitaji kuhakikisha kwamba vijana wanawajibika katika kujiendeleza ili kupata maendeleo chanya katika maisha yao, ili kufanikisha hayo vijana wanatakiwa kuwa na ufahamu na taaluma katika kuwezesha mabadiliko ya uchumi nchini Tanzania," alisema Rodriguez na kuongeza: "Vijana wasisahau kuwa wao ni chachu ya amani na maendeleo na UN tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha vijana wanakuwa wadau wa taratibu na kanuni zilizosababisha kuundwa umoja huu, wakijua na kutambua malengo ya dunia," amesema.
Rodriguez amesema UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo nchini.
"UN itashirikiana na serikali ya Tanzania kuleta maendeleo ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii," amesema.
Kwa upande wa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema serikali inatambua mchango wa umoja huo katika kuleta maendeleo nchini na kwamba itaendelea kushirikiana na umoja huo.
"Serikali ya awamu ya tano tangu kuanza kwake imefanya mambo mengi ili kuleta maendeleo, imedhibiti mianya ya ukwepaji kodi, imefanikiwa kutanua wigo wa ukusanyaji mapato na kuondoa rushwa. Hatuwezi kushinda pekee katika kuleta maendeleo ya wananchi, serikali iko tayari kushirikiana na jumuiya zote duniani," amesema.
No comments:
Post a Comment