Na Mary Margwe, Simanjiro
Imeelezwa kuwa baada ya kumaliza zoezi la kitaifa la ukamilishaji wa madawati kwa asilimia 100% katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara, sasa yageukia upande wa pili wa ujenzi wa madarasa,ambapo imelengwa zaidi kwa Shule za msingi ambapo ndio kwenye uhitaji zaidi.
Akiongea juzi katika mkutano wa baraza la Madiwani, kilichoketi chini ya makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Albert Msole, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Yefred Myenzi, Karibu tawala wa wilaya hiyo Zuwena Omary, alisema baada ya kuhitimisha suala la madawati sasa yageukia ujenzi wa madarasa.
Omary alisema wamefanya zoezi la uhakiki , na katika uhakiki huo wamegundua kuwa madarasa bado hayatoshi , kwa sababu katika uhakiki wao wamekuta chumba kimoja cha darasa linatumika kwa wanafunzi wa madarasa matatu yaani darasa la kwanza, na pili na tatu,ambapo hali imekua Mbaya zaidi kwa upande wa Shule za msingi.
Aidha alisema hali hiyo ni Mbaya katika kumjengea uelewa mtoto anayetakiwa kujengwa kitaaluma,hivyo ni vema hatua za haraka zinahitajika kukamilisha suala la madarasa kama lilivyofanikiwa zoezi la madawati, na hilo nalo likamilike kwa nijia hiyo hiyo.
"Ufaulu wa mtoto ni msingi gani tumemuwekea huyu mtoto,sio sisi kama wazazi tubaki kuhoji kufeli kwa watoto wakati wote,tujiulize na hili, kwani kufaulu ni pamoja na mazingira ya kujifunzia na kujisomea,baada ya kukamilisha hili sasa tuendelee kuhoji mengine mengi tu katika kuleta ufanisi katika kumjengea msingi bora" alisema karibu tawala huyo.
"Kwa hiyo wakati huutumemaliza utekelezaji wa madawati ambalo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, tena napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wilaya ya Simanjiro kiujumla kwa ambavyo tumefanikiwa, sasa twendeni tuhamie kwenye madarasa, haiwezekani na haikubaliki watoto wetu tukiendelea kuwaona wamekalia madawati mazuri, huku wakiwa wamerundikana madarasa matatu kwa moja (yaani three in one) alisema Omary.
Aidha alifafanua na kusema kuuwa katika suala hilo la madarasa hata waheshimiwa madiwani ni mashahidi katika kata wanazotoka wanajua dhahili kuwa hali ikoje, kwani ni mbaya hususani kwenye Shule za msingi,hivyo ni jukumu la Kila mmoja kuhakikisha anatoka kwenye baraza hilo akiwa na wazo jipya la ujenzi wa madarasa ambao ni wa lazima na si wa hiari.
Kufuatia hilo katibu tawala huyo alisema ni vema sasa uongozi wa wilaya ukajipanga wote kwa pamoja ,hukakikisha ni kwa namna gani zoezi hilo linakamilika ama kutekelezeka mara baada ya kujua ni madarasa mangapi yanahitajika,namna ya kupatikana kwake na kwa utaratibu gani.
"Mh.makamu mwenyekiti, kwa hiyo sisi tunasema wilaya yetu tujiunge wote kwa pamoja na tujikite zaidi kwenye ujenzi huu wa madarasa,hivyo tujiandae na sisi huku kama viongozi tunaweka mpango ambayo tutakubalina wote kwa pamoja kuwa nini kifanyike,tunahitaji madarasa mangapi na kupatikana kwake na kwa utaratibu gani na kwa muda gani" alisema karibu tawala.
Aidha aliwataka madiwani kwenda kuwaelimisha wananchi kwenye kata zao juu za zoezi hilo tarajiwa na kubainisha kwa namna gani wananchi watakavyoweza kushiriki kikamilifu katika utekelezaji na ukamilishaji wa zoezi hilo,huku lengo likiwa ni kuwajengea watoto misingi ulio bora wa elimu,kwani ufaulu wa mwanafunzi unaanzia kwenye msingi wake aliowekewa toka chini kabisa na so vinginevyo.
Hata hivyo, alisema hayo hayawezi kufikia malengo kwa kua na mpango wao pekee yake kama viongozi wa wilaya ama ofisi ya mkuu wa wilaya bila ya kushirikiana wote kwa pamoja, hivyo amewataka madiwani kuweza kuonyesha shauku za ujenzi huo katika kata zao.
"Darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanaanza ji imani yangu kuwa January mwakani,muda umekwenda sana,lakini ni imani yangu kuwa wote tunayo nia ya kuona watoto wetu wanasoma kwenye vymba au darasa stahili, kila wanafunzi wanakaa darasa lake, na Kila mwalimu anafundisha akiwa peke yake" alisema Omary.
"Lakini sasa hivi kinachotokea inawezekana mwalimu mmoja anafundisha akigeuzia watoto kile, na mwalimu mwingine anageuzia watoto wake upande huu,kwa hiyo anachoongea mwalimu huyu na wanafunzi wake, mwalimu mwingine na wanafunzi wake wanasikia (yaani vice verser) kwa hiyo na namna ya kuondokana na hili ni mi naomba wote kabisa tukubaliane kwa pamoja twende kwenye suala la madarasa,tujiandae na twende tukaanze kulitekeleza hili kwa ufanisi wa hali ya juu kabisa" aliongeza karibu tawala huyo.
Naye kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Albert Msole alisema madiwani hapaswi kukwepa wajibu wao, huo ni wajibu wao kinachotakiwa ni utekelezaji tu.Msole alisema kamwe hatarajii kuona diwani anakua chanzo cha kukwamisha shughuli yoyote ya maendeleo,likiwemo hilo suala la ujenzi wa madarasa ambalo limeongelewa na karibu tawala kwa kirefu zaidi.
"Madiwani wenzangu kama mlivyomsikia karibu tawala wetu,ametuelezea suala zima la ujenzi wa madarasa, sasa ni jukumu letu kuhakikisha suala hili tunaliunga mkono kwa asilimia zote, ili tufanikiwe kikamilifu" alisema Makamu mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment