1Baadhi ya watumishi wa TASAF wakisikiliza moja ya taarifa zilizotolewa kwenye mkutano uliopitia shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
1. Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.
1Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – umehitimisha mkutano wa wadau wa Maendeleo ambao wamepitia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru kaya maskini unaotekelezwa nchini kwa lengo la kuona utekelezaji wake katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Licha ya kuwa na mkutano , wadau hao wa maendeleo, maafisa kutoka baadhi ya wizara, taasisi za serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na watumishi wa TASAF walipata fursa ya kutembelea wilaya za Mbarali, Muheza,Chato,Mkulama na Pemba na kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona namna wanavyonufaika na ruzuku ya fedha inayotolewa kwa kaya maskini.
Majumuisho ya mkutano huo yameonyesha kuwa kuna mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mpango ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa walengwa kwa wakati, kuhamasisha walengwa kubuni miradi ya kujiongezea kipato na kushirikisha jamii katika utekelezaji wa shughuli za Mpango.
Aidha imeelezwa kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini na kuongezeka kwa mahudhurio ya watoto katika kupata huduma za kliniki mambo ambayo ni miongoni mwa masharti kwa walengwa kupara moja ya ruzuku zinazotolewa na Mpango wa Kunusuru kaya maskini.
Akizungumza mwishoni mwa mapitio hayo ambayo hufanyika kila baada ya miezi sita, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga ametaka jitihada zaidi ziendelee kuchukuliwa na wafanyakazi wa TASAF na wadau wengine wanaotoa huduma kwa kaya maskini ili walengwa waweze kunufaika na huduma za mpango.
Kwa upande wake Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Abdulahi Muderis amesema mafanikio yaliyoanza kuonekana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini ni kielelezo thabiti kinachoonyesha kuwa serikali ya Tanzania imo katika jitihada kubwa za kupambana na umaskini
No comments:
Post a Comment