Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza
kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya
Afrika Louis Rene Peter Larose (hayupo Pichani), makao Makuu ya Benki hiyo
Jijini Washington DC, Marekani, kulia kwake ni Katibu Mkuu w Wizara ya Fedha na
Mipango, Doto James.(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango).
Ujumbe wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania
wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya
Afrika, Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani), Makao Makuu ya Benki hiyo
Jijini Washington DC, Marekani, ambapo unafanyika Mkutano wa Mwaka wa Benki
hiyo ambayo Tanzania ni Mwanachama, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Sera
Augustine Ollal, Kamishna wa Bajeti John Cheyo na Kaimu Kamishna wa Fedha za
Nje Mamelta Mutagwaba.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya
Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC,
Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya
Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa inaiwezesha
Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango, wakishikana mikono kuonesha umoja na mshikamano mara baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, Jijini
Washington DC nchini Marekani, ambako ujumbe huo unahudhuria Mkutano wa Mwaka
wa Benki hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Katikati,
Akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya
Afrika mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo yaliyogusia Nyanja mbalimbali
za kijamii na kiuchumi, Jijini Washington DC, nchini Marekani, ambapo Tanzania
inashiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF.
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka
wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, baada ya kumalizika kwa
kikao kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia
anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, wakiwa nje ya
Majengo ya Benki hiyo Jijini Washington DC nchini Marekani. Wa kwanza kushoto
ni Kaimu Kamishna wa Fedha za nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta
Mutagwaba, Kamishna wa Bajeti, John Cheyo, Kamisha wa Madini James Andilile na
Kamishna wa Sera Augustine Ollal.
Wajumbe kutoka takribani nchi 180 duniani kote, wanachama wa
Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakiwa katika Siku ya kwanza ya
Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Jijini Washington DC nchini Marekani, Tanzania
inawakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango ambaye ameongoza
ujumbe wa wataalamu wa Fedha na Uchumi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (wa
kwanza kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili), Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania BOT, Prof Benno Ndulu (wa tatu kutoka Kushoto), Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Dkt. Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Kamisha
Msaidizi wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, wakiangalia
ripoti iliyotolewa na timu ya wataalamu wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha
Duniani-IMF, kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa
ufadhili na mkopo kutoka Taasisi hizo.
Ujumbe wa Tanzania na badhi ya viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha
Duniani-IMF wakikatisha Mitaa ya Jiji la Washington DC nchini Marekani kuwahi
vikao mbalimbali vinavyoendeshwa na Taasisi hizo kabla ya kufikiwa kwa kilele
cha Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Oktoba 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment