Na
Stella Kalinga Simiyu
Mwenge wa Uhuru umepokelewa ukitokea mkoani Shinyanga na kuanza mbio zake mkoani Simiyu, mkoa ambao kwa mujibu wa ratiba ni mwenyeji wa
kilele chake kitaifa tarehe 14 Oktoba mwaka 2016
Akitoa taarifa ya mkoa kwa Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 , George Mbijima Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka , amesema Mkoa huo unatekeleza kwa vitendo Ujumbe wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 inayosema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa,
Washirikishwe na kuwezeshwa’’ kwa kuwawezesha vijana wote kutekeleza
miradi ya maendeleo kupitia kauli mbiu
ya Mkoa wa Simiyu ya “Wilaya moja Bidhaa moja”.
Mtaka amesema Mkoa umewahamasisha vijana kujiunga
katika vikundi na kuwapatia mitaji katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuwa nchi ya Viwanda.
“Utekelezaji umeanza na Mkoa wa Simiyu tumejichagua
kuwa mkoa wa utekelezaji, Utekelezaji huo upo ambapo Wilaya ya Maswa ‘kwenye
wilaya moja bidhaa moja’ inazalisha chaki na Meatu inazalisha maziwa”, alisema
Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema kiwanda cha kuzalisha chaki cha
Wilaya ya Maswa kitafunguliwa rasmi na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge,Vijana, Ajira,Kazi na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb),
tarehe 10/10/2016 ambapo pia tarehe
11/10/2016 atafungua Kiwanda cha kusindika maziwa Meatu.
Aidha kuhusu ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge ; Serikali
Mkoani Simiyu kwa kushirikiana na wadau wengine katika kupambana na madawa ya
kulevya chini ya kaulimbiu ya “Tujenge jamii maisha na utu wetu;bila
dawa za kulevya” imeendelea
kutoa elimu na kuchukua hatua kwa wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya.
Katika Mapambano dhidi ya UKIMWI chini ya kauli mbiu
“Tanzania
bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI; Inawezekana”
Mtaka amesema mkoa unaendelea kutoa
elimu na kuwahamasisha wananchi kupima kwa hiari virusi vya Ukimwi ili waweze
kutambua hali zao na kujilinda na maambukizi mapya, kuachana na unyanyapaa na
kuzuia vifo.
Kuhusu mapambano dhidi rushwa chini ya kauli mbiu “Timiza
wajibu wako; kata mnyororo wa rushwa” Mtaka amesema TAKUKURU kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa inaendelea
kuwachukulia hatua wote wanaobainika kutoa na kupokea rushwa na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mapambano
dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja na kuelimisha kupitia klabu za wapinga rushwa
mashuleni.
Sanjari na hilo Mtaka pia amesema Mkoa wa Simiyu unaendelea
kupambana na Malaria chini ya Kauli mbiu “Wekeza katika Maisha ya baadaye; Tokomeza
Malaria” kwa kuwahamasisha wananchi kutumia vyandarua, kuua mazalia ya
mbu na kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapoona dalili za
ugunjwa wa malaria.
Mhe. Anthony Mtaka amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani humo utapita katika Halmashauri
sita (6) ukianzia Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Meatu, Itilima, Busega,
Bariadi na Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuona miradi minne (4), kufungua miradi tisa (9), kuweka jiwe la
msingi miradi sita(06) na kuzindua miradi 11 ya maendeleo katika sekta ya Afya,
elimu, maji, kilimo, barabara, sekta binafsi na utawala bora ambayo kwa ujumla
wake ina thamani ya zaidi ya bilioni 12.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) katika kijiji cha Wigelekelo
wilayani Maswa ukitokea Kishapu Mkoani Shinyanga.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016, Ndg. George Mbijima akivikwa skafu na
Vijana wa Skauti wa Wilaya ya Maswa kabla ya kupokelelewa na Viongozi wa Mkoa
Simiyu, akitokea mkoani Shinyanga
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2016, Ndg. George Mbijima.
Mkimbiza
Mwenge Kitaifa kutoka Mkoa wa Simiyu, James Munguji akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa mapokezi ya mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu
yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa.
Baadhi
ya Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakisalimiana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati
wa mapokezi ya mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu yaliyofanyika katika kijiji cha
Wigelekelo wilayani Maswa.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa kutoka Mkoa wa Simiyu, James
Munguji akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa mapokezi
ya mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo
wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisoma
taarifa ya Mkoa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016, Ndg. George
Mbijima katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa mara baada ya kupokea Mwenge
wa Uhuru kutoka Mkoani Shinyanga.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa tayari kushika Mwenge wa Uhuru mara baada
ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu
wa wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe.
Baadhi
ya wasanii wa Ngoma ya Wagoyangi kutoka Maswa wakitoa burudani kwa kucheza
ngoma wakiwa na nyoka aina ya chatu, mbele ya wananchi wa Wilaya hiyo waliofika
katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Wigelekelo.
No comments:
Post a Comment