Tuesday, October 4, 2016

NMB Mwanza ilivyosherehekea Wiki ya Huduma na wateja wake.

 Mmoja wa wateja wa NMB Tawi la Buzuruga, Consolata Shoto akikata keki kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnaba (wa pili kushoto) akimlisha keki mmoja wa wateja wa benki hiyo, Rachel Lububu kwenye tawi la NMB Buzuruga jijini Mwanza kwenye hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja. Baadhi ya wateja wa NMB Tawi la Buzuruga jijini Mwanza wakipata kifungua kinywa kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale (wa pili kulia) akikaribishwa kwenye Tawi la NMB Buzuruga jijini Mwanza na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnaba (kushoto) wakati alipofika kuzindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi hilo. Katikati ni Meneja wa Tawi la NMB Buzuruga jijini Mwanza, Justina Kikuli. Baadhi ya wateja wa NMB Tawi la Buzuruga jijini Mwanza wakipata kifungua kinywa kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Leonard Masale (wa pili kulia) akilishwa keki na Meneja wa Tawi la NMB Buzuruga, Justina Kikuli wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja Mwanza.

No comments: