Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva
(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, Taarifa ya
Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka
2015 kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini
Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva
(kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakionesha Taarifa ya
Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka
2015 ambayo ilikabidhiwa kwa Mhe. Waziri na NEC kwenye ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia kwenye mkutano wa
kukabidhiwa Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani wa Mwaka 2015, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva na Kulia ni Makamu Mwenyekiti
wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva
akitoa maelezo kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 ambayo aliikabidhi kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu
Mhe. Jenista Mhagama kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima
Ramadhani akitoa maelezo ya Utangulizi kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada
ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015, ambayo
Tume iliikabidhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) kwenye
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma
leo.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid
Mahmoud Hamid.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa makabidhiano ya Taarifa ya Tathmini
Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015
wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst.
Damian Lubuva (aliyesimama mbele).Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu
Mhe. Jenista Mhagama, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
Picha zote na Hussein Makame-NEC, Dodoma.
Christina Njovu-NEC, Dodoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi Taarifa ya
Tathmini baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani wa mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na
Walemavu Mh. Jenista Mhagama mjini Dodoma leo.
Akikabidhi taarifa hiyo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damin Lubuva alisema kuwa
Tathmini hiyo imeonesha kuwa Tume hiyo imefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuendesha na kusimamia uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba
25 mwaka 2015.
Alisema kwa mujibu wa tathmni hiyo Tume imebaini
kuwa sheria, kanuni na zilizotumika wakati wa Uchaguzi
mkuu zilikuwa chachu ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu,
Watendaji wa Uchaguzi walionesha kuwa na uelewa wa
kutosha wa Shriea na Kanuni za Uchaguzi.
Jaji Mst. Lubvuva alisema kuwa lengo la tathmini hiyo ni
kupata taswira halisi ya Tume kutoka kwa Wadau kwa
lengo la kujenga msingi bora wa utekelezaji wa chaguzi
zijazo na kujua kwa nini baadhi ya maeneo yalikuwa na
mwitikio mdogo katika kupiga kura wakati yalikuwa na
mwitikio mkubwa kwenye kuandikisha wapiga kura
kwenye Daftari la kudumu la Wapiga Kura.
Alisema kuwa Tathmini hiyo ni ya kwanza kufanyika
tangu kuanzishwa kwa Tume hiyo mwaka 1993 ambayo
imeweza kuwapatia mrejesho juu ya utekelezaji wa
Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau wa Uchaguzi .
Alibainisha kuwa wakati wa tathmini hiyo wadau wengi
walionesha kuridhishwa na utendaji wa Tume katika
kusimamia Uchaguzi Mkuu na kutangaza matokeo kwa
kufuata sheria na kanuni zilizopo.
Akipokea Taarifa hiyo , Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kwa kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu
ulikuwa na changamoto nyingi na ushindani mkubwa wa
kisiasa na kufanikiwa kufanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu
ambayo imekabidhia kwake kwa niaba ya Serikali.
“Ni kweli kwamba wananchi wengi wamekuwa na
mwamko wa kisiasa katika jamii yetu, hasa vijana , hivyo
taarifa hii itasaidia sana wananchi kuifahamu vyema zaidi
namna Tume inavyosimamia , kuendesha na kuratibu
mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hadi kutangaza
matokeo.” Alisema Waziri Mhagama.
Alisema Tathmini hii itawawezesha wadau mbalimbali
kuitumia kama nyenzo muhimu katika kushiriki na
kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan
Kailima katika maelezo ya utangulizi alieleza kuwa
tathimini hiyo ilitumia njia ya mahojiano ya ana kwa ana
na majadiliano na ilijumuisha makundi 192 ya wazee
wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na makundi 192 ya
vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35.
Alisema matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa kati
ya watendaji 1,029 walihojiwa na watendaji wengi kati
wao walisema taratibu mbalimbali za uchaguzi hadi
kutangaza matokeo zilizingatiwa.
Bw. Kailima aliongeza kuwa kuhusu Elimu ya Mpiga Kura
wadau wa Uchaguzi 1,915 waliohojiwa kuhusu uelewa
wao juu ya Elimu ya Mpiga Kura kati yao Wadau 1,463
sawa na asilimia 76.4 walisema kuwa walikuwa na uelewa
wa Elimu ya Mpiga Kura na Watu 452 sawa na asilimia
23.6 hawakuwa na uelewa.
Kutokana na tathmini hiyo Bw. Kailima alisema kuwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga kutoa Elimu ya
MpigaKura kwa lengo la kuwafikia wananchi na wadau
moja kwa moja na imeweza kushiriki katika maonyesho
mbalimbali yakiwemo ya Sabasaba, Nanenane , Mkutano
wa Tawala za Mitaa Tanzania na Wiki ya Vijana
iliyofanyika Mkoani Simiyu.
Sambamba na hilo, aliongeza kuwa Tume imepanga
kuhudhuria na kutoa Elimu katika mikutano ya viongozi
mbalimbali ikwemo viongozi wa Dini, Mabaraza ya
Madiwani na mikutano mikuu ya vijiji na mitaa.
Kutoa elimu ya Mpiga Kura kwa njia ya luninga, redio,
mabango na mitandao ya kijamii, Kutoa vibali vya kutoa
elimu ya Mpiga kura kwa Taasisi na Asasi.
Kufanyika kwa tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 ni mojawapo ya
ukamilishaji wa mzunguko wa Uchaguzi huo ambao
ulitanguliwa na zoezi kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa Mh. Rais Wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Ikulu jiji Dar es Salaam na ni
mwanzo wa kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi
mwingine.
No comments:
Post a Comment