Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja
akisalimiana na baadhi ya Maafisa Watendaji katika mradi wa Uzalishaji
kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Mkoa wa Pwani leo
Oktoba 28, 2016 alipotembelea mradi huo ili kujionea shughuli za uzalishaji
wa kokoto.
Meneja Msaidizi wa Mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo
Pongwe Msungula, Kepteni Gaspa Rugayana akitoa maelezo mafupi
kuhusiana na mradi huo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John
Casmir Minja(kulia).
Ujumbe wa Maafisa Watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la
Magereza(Prisons Corporation Sole) ambao umefuatana na Kamishna
Jenerali wa Magereza katika ziara ya mafunzo kwenye mradi wa Uzalishaji
kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Mkoa wa Pwani. Shirika la
Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto
katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Maafisa Watendaji wa SUMA – JKT katika mradi wa Uzalishaji kokoto
wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula wakimtembeza katika maeneo
mbalimbali Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(wa
tatu kulia) alipofanya ziara ya mafunzo katika mradi huo(kulia) ni Meneja
Fedha na Utawala katika Mradi huo, Bi. Glory Kimaro.
Meneja Uzalishaji wa mradi wa kokoto, Kepteni Paul Mbeya
akimuonesha mtambo wa uzalishaji kokoto Kamishna Jenerali wa Magereza,
CGP- John Casmir Minja(kulia).
Mtambo wa Uzalishaji katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA –
JKT uliopo Pongwe Msungula kama unavyoonekana katika picha. Shirika la
Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto
katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Meneja Mkuu wa Mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT, Bw.
Semih Yaran akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John
Casmir Minja(wa pili kulia) maeneo mbalimbali ya mradi huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia)
akiangalia kokoto za kutengenezea barabara zinazozalishwa katika mradi
huo. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa
Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Muonekano wa kokoto zinazozalishwa katika Mradi wa Uzalishaji
kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Musungula(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment