Saturday, October 15, 2016

MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA MBIONI KUMALIZIKA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa jijini humo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela kabla ya kuyafanyia urasimishaji na kutoa hati ya makazi kwa wamiliki wake.

Kiomoni alifanya ziara ya kutembelea Kata za Buhongwa na Luchelele na kuzungumza na wakazi wa kata hizo juu ya maeneo yenye migogoro na ambayo bado wananchi wanadai fidia ili kutatua changamoto hizo.
Na BMG
Diwani wa Kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi (mwenye suti) akizungumza kwenye ziara hiyo na kuelezea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Kata yake kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi kabla ya urasmishaji wa makazi yaliyojengwa kiholela kufanyika katika kata hiyo. 
Wengine ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo watendaji wa idara ya ardhi.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa ambaye kiwanja chake kina mgogoro akitoa malalamiko yake mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Hatimaye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza aliahidi kumpatia kijana huyu kiwanja kingine ili kuondokana na kiwanja hicho chenye mgogoro.
Wakazi wa Kata ya Buhongwa Magharibi Kata ya Buhongwa wakiwa kwenye kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kilicholenga kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Wakazi wa Kata ya Luchelele Jijini Mwanza
Diwani wa Kata ya Luchelele, Vicent Lusana, akizungumza katika mkutano huo ambapo alihimiza halmashauri ya Jiji la Mwanza kulipa fidia kwa wakazi wa kata hiyo kwani ni muda mrefu tangu zoezi la uthamini wa ardhi ulipofanyika katika Kata hiyo.
Alfredy Ngendelo ambaye ni Mthamini wa Jiji la Mwana, akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata Luchelele kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia baada ya uthamini kufanyika.
Afisa ardhi mteule Jijini Mwanza, Halima Nassor, akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Luchelele wakiuliza maswali ikiwemo kulipwa fidia baada ya zoezi la uthamini wa ardhi yao kukamilika muda mrefu bila kulipwa fidia, ambapo waliombwa kulipwa fidia zao mapema ili waondoke katika maeneo yao ambayo yamepimwa kwa ajili ya miradi ya kijamii.
Baadhi ya maeneo hatarishi yenye miinuko ambayo Mkurugenzi wa Jiji Mwanza amezuia ujenzi wake kuendelea.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.

Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanza zoezi la kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela ili kuyafanyia urasimishaji.


Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema zoezi hilo limelenga kuondoa migogoro yote ya ardhi na kutoa hati ya makazi kwa wananchi ambao makazi yao yaliyojengwa kiholela yatarasimishwa.

Amesema wale waliojenga katika maeneo hatarishi ikiwemo milimani, hawatahusika katika zoezi hilo hivyo wasiendelee na ujenzi wa makazi hayo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa na Luchelele, wameomba migogoro yote ya ardhi inayowakabili ikiwemo kulipwa fidia katika maeneo yao, itatuliwe kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya tathmini upya na katika maeneo yenye migogoro na kutoa hati za umiliki.

Zoezi hili limejili ikiwa siku chache baada ya Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, kufanya ziara Jijini Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kutembelea maeneo yote yenye migogoro na makazi holela kabla ya zoezi za usaminishaji kufanyika.

No comments: