Afisa
Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiwaeleza
wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF ikiwa ni
pamoja na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambapo mtu yeyote mwenye umri wa
kuanzia miaka 18 anaweza kujiunga na kunufaika na mafao mengi.
Baadhi
ya viongozi na watumishi wa Hoteli ya Heritage wakiwa wanasikiliza kwa makini
somo kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji
Jamadary kuhusu mafao yatolewayo na mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Mmoja
wa wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage akiwa anasoma jarida kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF
Afisa
Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akigawa vipeperushi
na majarida yanayoelezea kwa kina huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo.
Wafanyakazi
wa Hotel ya Heritage wakiwa wanachukua fomu kwa ajili ya kujiunga na Bima ya
afya ya NHIF itolewayo kwa Bei nafuu kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari
(PSS)
Baadhi
ya watumishi wa Hoteli ya Heritage Jijini Dar es salaam wakiendelea kusoma
vigezo masharti na mambo mbalimbali juu ya Bima ya afya ya NHIF inayotolewa
kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Wafanyakazi
wa Hoteli ya Heritage wakiendelea kupata maelezo juu ya Mfuko wa Pensheni wa
PSPF kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji
Jamadary
Picha
na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea
kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo.
Hayo
yamesemwa na Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Hadji Jamadary alipokuwa akitoa maelezo na mafunzo juu ya mfuko huo na
wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage iliyopo Jijini Dar es
salaam ambapo pamoja na kutoa maelezo juu ya mfuko huo na
kutoa elimu ya juu ya mpango huo wa uchangiaji wa hiari
ambapo mwanachama atatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 ,
atakuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha
chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki
na huduma za simu.
Bwana
Hadji alisema kuwa mpango huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila
kusahau mjasiriamali na mfanyakazi wa serikali na kuongeza kuwa
mwanachama anayejiunga katika mfuko huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo
ni; Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la
Ugonjwa/Ulemavu, Fao la Kujitoa, na Fao la Matibabu.
Akifafanua
kuhusu Fao la Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa
uchangiaji wa hiari wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
ambapo mwanachama ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya
madawa yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.
“Mwanachama
anaweza kuwasajili pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu
bila shida yoyote,” alisema Hadji
Wakizungumza
kwa nyakati mbalimbali wafanyakazi hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo
na kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge
kwa kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko
huo.
Aidha
Hadji aliwaambia wafanyakazi hao kuwa PSPF ina wawezesha wanachama
wake na jamii kwa ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora,
Mtwara, Shinyanga na Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara
moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment