Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa
zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya
kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
Shukrani na Pongezi
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili Kijijini Mtamaa kwa ajili ya mkutano na kukabidhi
kifaa maalumu kwa ajili ya kupimia Malaria
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
Baadhi ya wananchi wakifurahia kifaa cha kupimia Malaria
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano
Na Mathias Canal, Singida
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo
cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za
upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.
Tatizo
hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa
kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.
Mhe
Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson
Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho
ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua
kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka
jana.
Sima
alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere
kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa
kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.
Sima
Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo
mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa
katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi
na uhuru wa maendeleo.
Alisema
kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni
pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani
katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.
Sima
ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya
Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa
vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.
Kuhusu
kadhia ya uduni wa upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A
Mbunge huyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa
yameanza kutoka ili kumaliza kadhia hiyo kwani mradi mkubwa wa maji
utakuwa umemalizika.
Kwa
upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye
pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo
kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani
huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.
Chima
amesema kuwa Mbunge huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi
wake na ameonyesha uwezo mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kutetea hoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji.
Naye
mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa
kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni
madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa
muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda
kupima ugonjwa huo.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Maadhimisho
ya Mwalimu Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote
ulimwenguni huadhimisha kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya
heshima kwa muasisi wa Taifa lao.
No comments:
Post a Comment