Friday, October 14, 2016

KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAZINDULIWA RASMI ENEO LA PAKACHA KATA YA TANDALE JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo akizindua rasmi kampeni ya Binti wa Kitaa
Binti Zawadi Mansende  akizungumzia anayesoma Shule ya Sekondari ya Manzese Kidato cha Tatu akizungumzia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kama wasichana wa mtaani ikiwa ni pamoja na kurubuniwa na Vijana jambo linalowapelekea kukumbia majumbani mwao na wengine kupata Mimba za utotoni, wakati wa uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa.
Baadhi ya Mabinti waliokati ya umri wa miaka 14 na kuendelea wakiwa wanafuatilia kwa makini uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa iliyofanyikia Tandale
Baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa wanaonesha #tag  Binti ya Kitaa.
Baadhi ya wadau na Mabinti wa Kitaa wakiwa katika uzinduzi huo
Bwana  Godfrey Nteminyanda ambaye ni Mkurugenzi wa Applemackbooks_tz akielezea namna alivyo ipokea kampeni hiyo na wao kuahidi kuisapoti kwa hali na mali
Baadhi ya akina mama wa Tandale pamoja na waendeshaji wa Kampeni ya Binti wa kitaa wakiwa katika uzinduzi
Mama Consalva Genes Samba ambaye ni Mkazi wa mda mrefu wa Tandale akielezea namna mabinti wamekuwa wakirubuniwa na kudanganywa .
Baadhi ya wawezeshaji, na wakazi wa Tandale wakionesha Mabango ya Binti wa Kitaa
Madam Sophia Mbeyela akizungumza jambo wakati wa Uzinduzi huo
Ulifika Muda wa kupata mambo ya Kitaa yaani Bagia, Vitumbua Chachandu na Ujii ilikuwa ni safi sana
Hawa ni Baadhi ya Timu ya waandaaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa
Hii ni timu nzima ya kitengo cha habari cha Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi kuisha
Tukio likiwa linaendelea
Pamoja na kuwa ni Kampeni ya Binti wa kitaa wanaume nao wamehamasika kuisapoti mwanzo mwisho hapa wakiwa pamoja na Mabinti wengine wanaosapoti.
Picha ya pamoja  .Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani

Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF)  imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni  nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.

"Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema  George.

BINTI WA KITAA  imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.

Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.

Kadhalika mmoja kati ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo Zawadi Isihaka ameomba wazazi kufuatilia maendeleo na kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuyagundua mapema mabadiliko ya tabia pamoja na kuwapa elimu ya makuzi sambamba na kutokuwa wakali kupitiliza kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo waratibu wa eneo ambao ni Tandale Youths, Applemacbooks Company,wakazi wa eneo la Pakacha ,Tandale, waandishi wa habari pamoja.

Sambamba na uzinduzi huo katika kata ya Tandale,Ndg. George David ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono kampeni hii  ili kuweza kuwasaidia mabinti kwani ni wazi kuwa hili limekuwa sehemu kubwa ya kuzalisha wimbi kubwa la watoto wa mitaani, vifo wakati wa kujifungua, athari za kisaikolojia na kiuwanyima mabinti nafasi ya kupata haki yao ya msingi ya elimu. 

No comments: