Friday, October 7, 2016

Kwa nini Afya call Health Services?

AFYACALL ni nini?

Afya call ni kampuni  iliyobobea katika utoaji huduma wa ushauri wa kitabibu kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu. 
Lengo letu ni.
- kusaidia upatikanaji wa huduma ya ushauri wa kitaalamu juu ya afya kwa wananchi wote ikiwemo wale walio maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa kuwa na miundombinu mibovu
- kusaidia wanaoishi mbali na huduma za haraka za hospitali ama wataalamu wa Afya .
-kuunga mkono juhudi za serikali yetu katika kuboresha huduma za Afya na kupunguza idadi Ya vifo vitokanavyo na kukosekana Kwa ushauri wa kitatibu na huduma ya kwanza.
Huduma zetu za ushauri  Kwa nji ya simu zinapatikana kwa masaa 24, siku 7 za wiki ukiwa mahali popote ndani ya Tanzania

Huduma zetu zinatolewa Kwa gharama nafuu sana kuwezesha wenye kipato cha aina zote kunufaika nazo.
-* Kwa elfu 20 Tu utaunganishwa  Kwa mwaka mzima unapata huduma za ushauri Bure na ukishajisajili unaweza kupiga simu Bure bila makato wala gharama yoyote muda wowote ule*( gharama hii ndogo ni kuchangia uendeshaji na malipo ya wataalam / madaktari )

Madaktari wetu wote wamethibitishwa na baraza la madaktari wa Tanganyika (MCT)
Kwa nini Afya call Health Services?

Katika mazingira yetu wataalamu wengi wa afya wanapatikana katika miji mikubwa, matokeo yake eneo kubwa la nchi yetu hususan vijijini yanakosa huduma za afya. Afya call inaondoa utofauti huu katika kupatikana kwa huduma za afya kati ya mijini na vijijini. Pamoja na faida nyingine Afya call itaisaidia kufikia lengo la serikali la ‘kuwezesha upatikanaji wa huduma sahihi za kiafya kwa njia ya kielektroniki kwa wagonjwa wa maeno ya pembezoni na jamii na za vijijini.’

Inafanyaje kazi?
• Kituo chetu cha kupokelea simu kina manesi ambao watapokea simu ya mteja na kumsikiliza kisha kumuunganisha na Daktari kutokana na hitaji lake la kiafya.
• Muda wote wa saa 24 siku zote saba za wiki kutakuwa na huduma ya madaktari
• Kuwaelekeza wagonjwa kwenye vituo vya afya vilivyo karibu nao inapolazimika.
• Kuhamasisha mwenendo wa kujua hali za kiafya kwa kuwapa taarifa za ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu zao za mkononi.
• Huduma zitatolewa kwa njia ya simu hivyo kupunguza msongamano usio wa lazima kwenye hospitali.

Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kujiunga tupigie Namba 022 5508200 .
Website ; www.afyacall.co.tz
Facebook /Twitter ; AfyaCall

No comments: