Monday, October 24, 2016

Kamoga ataka watendaji, madiwani kumpa ushirikiano

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara,Hudson Stanlay Kamoga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mikakati aliyojiwekea katika utendaji wake wa kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo..Picha na Mary Margwe.
Na Mary Margwe, Mbulu


.Ndoto yake ni kuibadilisha Mbulu kuwa nchi ya vitunguu swaumu.(Mbulu the land of garlic).Asisitiza mambo muhimu matatu ya kuleta mabadiliko ya maendeleo yanayotokana na neno P I A

P---Patriotism---Uzalendo
I----Integrity. ----Uadirifu na
A---Accountabiliyt---Uwajibikaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini,Mkoani Manyara , Hudson Stanley Kamoga, amewataka watendaji,madiwani na wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia wananchi Wilayani humo kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo.

Akiongea na waandishi wa habari Jana ofisini kwake, Kamoga alisema ushirikiano katika nyanja yoyote ile inahitajika ili kufikia malengo,hivyo naye anaomba apewe ushirikiano ili kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika kuhakikisha Mbulu unajua na maendeleo ya kweli na si vinginevyo.

Kamoga alisema ushirikiano huo uende sambamba na kuwataka wakuu wa idara kumpa mpango kazi wake wa mwezi mmoja kuwa mini amefanya kwenye idara yake, kama idara wamekutana na vikwazo / changamoto gani na ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo

Kamoga alisema yeye kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbulu, angependa kuona madiwani na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo wakiwa wanazungumza lugha moja tu ya maendeleo na si vinginevyo.

"Lazima kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu,nihakikishe watendaji na madiwani wanafanya kazi kama timu moja, kwani siku zote umoja ndio hujenga kitu chochote cha maendeleo na msingi wa maendeleo ni ushirikiano yaani umoja,hivyo uwezo ninao wa kulisimamia hili na hatimaye kuweza kuona tuko wapi, tumetoka wapi na tunatarajia kwenda wapi " alisema Kamoga.

Aidha alisema ili kufikia malengo aliyojiwekea kikamilifu, ametengeneza utaratibu ambapo angependa watendaji wake wote wa halmashauri waufuate na kuuzingatia kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kila siku.

"Wanahabari kuna hili neno lenye herufi tatu tu lakini lina maana kubwa sana katika utekelezaji wa majikumu yetu ya Kila siku ambapo tukilishika kikamilifu hakuna kitakachokwenda mrama,ambalo linasomeka P I A , P ...limesimama kama neno Patriotism (Uzalendo) , herufi ya pili ni I...limesimama kama Integrity (uadirifu) na la tatu ni A...ambalo limesimama kama Accountability (Uwajibikaji).

Kamoga alifafanua kua kufuatia maana ya neo PIA, anataka kutengeneza halmashauri yenye watendaji wazalendo, na hao wazalendo lazima wabebe uadirifu kisha tatu Uawajibikaji ,hawa wazalendo ambayo ni waadirifu lazima wawe waajibikaji ,ambapo alisema kukishakua hivyo katika Kila idara zote ambazo watendaji wake wako hivyo, halmashauri hiyo itapiga hatua kubwa mbele kimaendeleo katika kukabiliana na changamoto zilizopo.

" Kwa hiyo wote tuibebe neno P I A ili tuwe wazalendo, waadirifu na pia tuwe waajibikaji Kila mmoja ahakikishe ana anawajibika kwenye nafasi yake wa uwezo wake wote ,hapo tutasonga hatua mbele kimaendeleo,hii ndio misingi yangu ninayotaka tujijengee na watendaji wangu wa halmashauri

Je? Ni Mikakati gani ambayo itamwezesha Kamoga kufikia malengo yake?

Kila mmoja atahakikisha anafanya kazi kwa mazingira yake bila kuingiliana na mwingine,ambapo ana amini madiwani kwa moyo na uchu walionao wa kutaka maendeleo katika jamii hususani ndani ya kata zao.

Aidha alisema kubwa madiwani watashirikiana kwa umakini kabisa na watendaji walipo kwenye kata hadi ngazi ya vitongoji vyao, ili kuhakikisha wanapunguza migogoro iliyopo vijijini na kwenye kata zao katika kuleta maendeleo ndani ya kata na vijiji, " Lakini pia watendaji wangu wafanye kazi kwa uzalendo, uadirifu na Uwajibikaji wa hali ya juu, hii ndiyo mikakati yangu .

Pamoja na hayo yote lakini je? Nini Ndoto zake za baadaye kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kama Mkurugenzi??

"Ndoto yangu kubwa nataka na natamani kuona watu wa ndani na nje ya nchi yaani Tanzani na duniani kote ijue kuwa Mbulu ionekane kama nchi ya vitunguu swaumu ( The land of Garlic) kule Bashay na Mbulu kiujumla tunazalisha vitunguu bora huku wananchi wake bado wanaonekana kutonufaishwa na zao hili" alisema Kamoga.

Alifafanua kuwa lengo vile vitunguu vibadilike kubadilisha maisha wana Bashay ,wakulima wafurahie uwepo wa uzalishaji mkubwa wa vitunguu swaumu,ambapo alibainisha vitunguu vinavyosafirishwa kwenda nje ni vema viende vikishakua vimewekwa lebo kuonyesha hili ni zao la MBULU ( this is the product of Mbulu / Mbulu product) .

"Hiki ndicho natamani sana sana ,kwa hiyo mtu anakula kitunguu swaumu akiwa anajua kabisa kuwa anakula kitunguu cha wapi , mtu yoyote akienda sokoni moja kwa moja aulize nataka kitunguu cha Mbulu, huu ndio ufahari wangu,nitasimamia kuhakikisha hili linatekelezeka" alisema Kamoga.

No comments: