Thursday, September 15, 2016

Zijue tofauti za mitindo ya karate na sanaa nyingine kuu za mapambano 7 toka Japan

Na Sensei Rumadha Fundi
Hapana  budi , bali ni furaha kuielimisha jamii ya wapenda karate na sanaa mbali mbali za mapambano na kujilinda zenye asili ya Japan. Ingawa ni vigumu kuchambua historia zake zote kiundani, bali muktasari wake unawezekana na kuipa jamii ya mapenzi ya hizi sanaa mpambazuko wa ufahamu kuhusu sanaa hizi za Kijapan. Katika muktasari huu, itaongelewa zile sanaa halisi ( original) au shina lake na siyo matawi ya baadhi ya sanaa hizi yaliyojitokeza baada ya waanzilishi kufa na wanafunzi kuanzaisha mitindo yao.

1.     JUDO 2. KENDO 3. AIKIDO 4.JUJUTSU 5. KEMPO  6. KOBUDO 7. KARATE.

1.     Judo: Yenye maana “ Mwenendo wa sanaa ya upole”Mieleka  ilianzishwa mwaka 1882, kama mazoezi ya mwili na fikra kuimarisha mwili kuwa madhubuti au imara. Mwanzilishi wa sanaa hii ya Judo ni mkufunzi wa Buddha “Buddhist” Jiogoro Kano, kwenye hekalu la “Eisho-ji”Buddha kama dojo yay a Judo mjini Tokyo. Papo hapo ndipo na miaka miwili baadae kuanzisha chama cha Judo kiitwacho “Kodokan”kikimaanishe au tafsiri, “Sehemu ya kuonyesha njia”. Kipindi hicho, Sensei Kano alikuwa bado hajapewa “ Menkyo” au kumuenzi na cheo cha master.

2.     Kendo: Yenye maana “ Njia ya upanga” ni sanaa nyingine pia ya Japan yenye kutumia mapanga kwa kujilinda na kushambulia pia.


3.     Aikido: Ni saa ya kisasa pia ilianzishwa na  Morihei Ueshiba, ikiwa na maana, “ Njia ya kuunganishanisha nafsi na roho”, ama pia “ Njia ya kuunganisha nguvu za maisha”. Master Ueshiba , alibuni mbinu hizi za kujilinda kutumia nguvu za  kumrusha  mpinzani wako wakati akigoma na kuigeuza nguvu yake mwenyewe kumzatiti na kupinda viungo kummiliki mpizani. Aikido, ilianzishwa mnamo miaka ya 1920 ikiwa nimoja ya ndoto zake toka katika dini yake ya  kidini ya “Omoto - Kyo”. Leo Aikido, anafundishwa duniani kote na ina matawi tofauti ya mfumo wakufundisha.


4.     Jujutsu: Jina Jujutsu, halikutolewa hadi hapo mnamo mwanzoni mwa karne ya 17, ikiwa mbinu zake zime sambaa kiujumla kama miekeka, na hali kadhalika kunyongana na kikiri kiri na kiujumla ni mzunguuko kamili wa kujilina kwa karibu na mpinzani kimwili kuwa pamoja au mapambano ya karibu ya kugusana. Kiujulma ni kwamba, Jujutstu ina husisha mbinu nyingi tofauti zikiwemo kushambulia, ngumi, kumrusha adui, kumbana adui, kunyonga adui, na hata mieleka pia.
Sanaa hii inachimbuko lake Japan na baadae kutambulishwa Brazil mwaka 1914 na sensei Mitsuyo Maeda, ambae moja ya wanafunzi wake toka Brazil ni Sensei Carlos Gracie na familia yake walikuja endeleza sanaa hii kupitia michezo na kujulikana kama “Gracie Jui Jutsu” au pia maarufu kama “Mixed Martial Arts”. Upo ushawishi mwingi sana toka katika mfumo wa Jigoro Kano Judo, ambaye ndiyo “Baba wa Judo” Maste Kano ndio aliyekuwa mwalimu wa Sensei Mitsuyo Maeda na kusambaza Ju Jutsu hadi Brazil.

5.     Kempo: Kutokana na historia yake, Kempo ililetwa China na mwanzilishi wa Zen, Boddhidarma mnamo karne ya 1500. Baada ya kuondoka India kufundisha “Buddhism” China. Safari ya Buddha, iliishia katika hekalu la Songshan, kwenye Hekalu maarufu la “Shaolin”, ambapo leo kunajulikana kama jimbo la “Henan”, na baadae mbinu hizo kuenea nchi yote ya China.

Hii sanaa ya Kempo, yenye maana ya “Boxing”, imejigawa katika makundi matatu tofauti na miaka iliyopisha  kwa wakati wake. Sanaa hii ili pelekwa katika visiwa wa Okinawa na inauhusiano mkubwa sana na mtido wa “Shuri Te, Shorinji Ryu  na Shorin Ryu, Shito Ryu, Motobu Ryu” pia. Sababu ndio mtindo aliotoka nao Master Gichin Funakoshi
( Shuri Te) toka Okinawa kwenda Japan ya bara 1922, na baadae kuitwa Shotokan Karate.

6.      Kobudo: Sanaa ya kutumia silaha asili za Okinawa. Ikiwemo , Nunchaku, Sai, Tonfa, Bo,Kama, ngao, upinde, mwiko wa ngalawa  nk. Sanaa hii inatambuliwa kwa kuitwa “ Njia ya sanaa ya mapambano asilia ya zamani ya Okinawa”. 
7.  Karate & Okinawa
Chimbuko la Karate ulimwenguni ni  Okinawa, Japan. Mwaka 1429 falme tatu za  Ryukyu ziliungana na kuunda utawala wa visiwa vya Ryukyu. Wakati mfalme  Sho Shin kaja kwenye madaraka, 1477, alifungia mafunzo na harakati zote za sanaa ya Karate visiwani humo. Hivyo kuwa sasa watu walipaswa kuwa wanafanya mazoezi ya sanaa kwa siri na kujificha iwezekanapo toka kwa wenye mamlaka. Ilifungiwa hadi hapo mwaka 1609 baada visiwa hivyo kuvamiwa na jeshi la “Satsuma “ la Japan. Hapo ndipo palipochangia sana kuanzishwa kwa “Kobudo” utumiaji vifaa asilia kuvibuni kama silaha na kuwa na mazoezi ya siri huku wakiendeleza mbinu za juu. Huo pia ulikuwa mwanzo wa kubuni “Mikono ya Okinawa” au “Okinawa Te”. Hadi kufika karne ya 18, wilaya zote tatu yaani, Shuri, Naha na Tomari za Okinawa ziliendeleza mitindo yao tofauti ya mbinu za mikono mitupu kwa wakati huo.

Mitindo ya iliitwa, Shuri te, Naha te  na Tomari te.

Machimbuko ya mitindo kuzaliwa kutokana na miji hii mitatu.
Shuri te: Toka mji mkuu wa visiwa vya Okinawa Shuri ambako ndipo mfalme wa Ryukyu aliishi kwenye “Shuri Castle”.
Waalimu wakuu maarufu wa Shuri te:
Yamaza  Yamazu, Itosu Anko, Asato Anko, Choyu Motobu, Motobu Choki, Gichin Funakoshi, Kenwa Mabuni, Tatsuo Shimabuku.
Kata zake:
Naihanchi, Pinan, Kusanku, Passai, Jion, Jitte, Rohai, Chinto, na Gojushiho.
Mitindo iliyozaliwa toka Shuri te   ni:
Shotokan,  Shito Ryu, Shorin Ryu, Shudokan, Shorinji Ryu, Gensei Ryu na Motobu Ryu.
Tomari te toka mji wa Tomari:
Waalimu maarufu toka huko ni:
Matsumora Kosaku, Motobu Choki, Kyan Chotoku na Oyadomari Kokan.
Kata za Tomari te:
Naihanchi, Eunibu, Rohai, Wanduan, Passai, Chinsu, Chinpu, Wankan, Wanshu, Seisan, Jumu, Nichin, na Juma.
Mitindo iliyozaliwa baada ya hapo toka Tomari te  ni:
Wado Ryu, Motobu Ryu, Matsubayashi Ryu, na Shorinji Ryu.

Naha te toka mji wa Naha ambapo ndio mji mkuu wa visiwa vya Okinawa kwa sasa baada ya kuwa sehemu ya Japan.
Waalimu wa kuu maarufu toka Naha:
Arakaki Seisho, Kanryo Higaonna ( Higashionna), Chojun Miyagi, Kyoda Juhatsu, Kenwa Mabunu, Uechi Kanbun.
Kata za Naha te:
Sanchin, Saifa, Seiuchin, Shisochin, Seipai, Seisan, Sanseiru, Tensho, Kururunfa, na Suparinpei.
Mitindo iliyo zaliwa toka Naha te:
Okinawa Goju Ryu, Uechi Ryu,na  Shito Ryu.
Imenukuliwa na Sensei Rumadha Fundi, mkufunzi wa Karate  kwa zaidi ya miaka 38 mwenye ujuzi wa ngazi ya juu na uzoefu wa kimataifa  mpaka sasa ana  6 Dan TKF, 3 Dan (Jundokan So Honbu)  2 Dan (Goju Ryu Kyokai) ambaye amenufaika kufanya mafunzo chini ya Morio Higaonna sensei, Teruo Chinen sensei, Matasaka sensei, Gima na Kinjo sensei, Kazuya Higa sensei, Yasuda sensei na Kancho Miyazto sensei pia. Hii inatoka katika makumbusho ya Karate Okinawa, Japan.



















No comments: