Friday, September 23, 2016

WANAFUNZI ZANZIBAR WAFANYA SHEREHE ZA ELIMU BILA MALIPO ZANZIBAR.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma wakati alipodhuria katika Maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikaribishwa na Katibu Mkuu   Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi Khadija Bakari mara alipowasili katika   Maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo, sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi mara alipowasili katika   Maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo, sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe zaa  maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo   zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd,Mmanga Mjengo Mjawiri (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa katika sherehe za miaka 52 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studum Mjini Unguja,mgen rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Walimu wa Skuli mbali mbali za Unguja na Pemba wakiwa katika sherehe za miaka 52 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studum Mjini Unguja,mgen rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studum Mjini Unguja,mgen rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studum Mjini Unguja,mgen rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Wanafunzi wa Skuli ya Mwanakwerekwe D,wakiwa katika maandamano ya sherehe za Elimu  bila Malipo zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studum Mjini Unguja,mgen rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),na kuhudhuriwa na wananchi mbali mbali.
 Wanafunzi wa Skuli ya SOS  wakiwa katika maandamano wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 52 ya Elimu Bila Malipo, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja
 Wanafunzi wanawake wa Skuli ya Ben Bella Secondary wakiwa katika maandano kusherehekea miaka 52 ya Elimu bila Malipo sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  Wanafunzi wa Skuli za Mkoa wa Mjini Magharibi wakibeba bango lilalotoa ujumbe kumpa “heko Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuimarisha Elimu na Michezo”wakati wa maandamano ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila Malipo,sherehe zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Wanafunzi  wa Skuli za Mkoa wa Kaskazini Pemba  wakiwa katika maandano kusherehekea miaka 52 ya Elimu bila Malipo sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 23/09/2016.

NA  TAKDIR ALI. MAELEZO ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuifanyia ukaguzi mitaala ya Skuli za binafsi ili kwenda sambamba na mitaala ya  Skuli za Serikali.

Hayo ameyasema leo huko Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akihutubia wananchi  katika maadhimisho ya miaka 52 ya elimu bila malipo.

Amesma mitala ya skuli za binafsi haiendi sambamba na ile ya serikali kitu ambacho hakipaswi ,hivyo amesema  ikohaja ya Wizara ya elimu namafunzo ya amali Zanzibar kushirikiana katika kuangalia mitaala miataala hiyo ya ufundishaji  ili iende sambamba  na skuli za serikali.

Aidha amesema  mashirikiano ya pamoja yapande hizo mbili yatapelekea wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya majaribio na ile ya mwisho wa mwaka.

Dkt. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba  inakabiliana na changamoto mbalmbali  zinazoikabili sekta ya elimu hapa Zanzibar ili kuhakikisha inafikia dhana ya Raisi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alioitangaza Elimu bila malipo  mwaka 1964.

Akiwazungumzia Wazazi juu ya suala zima laelimu kumpatia mtotoDkt. Ali Mohamed Shein amesema suala la elimu kwa mtoto hali mlazimu mwalimu pekeyake bali ni jambo la wote  ambalo linahitaji ushirikiano kati ya mwalimu wazazi na wanafunzi.

Amesema wasiachiwe walimu pekeyao kufundisha na kuwaongoza bali wae na ushirikiano wa pamoja.

Pamoja na hayo  Dkt.Ali Mohamed Shein alisema kabla ya Mapinduzi ya Mwaka1964  ilimu Zanzibar ilikuwa ikitolewa kwa misingi ya ubaguzi kituambacho kiliwafanya wonyonge kuikosa hakihiyo ya elimu  kitu ambacho  kwa sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa mbele kwani upatikanaji wa elimu ni wakila mmoja ambae kafikia umri wa kwenda skuli.

Ameseama haki hiyo sasa imefikiwa kukua nakwasaa kua na vyuo vikuu vitatu kwa ujumla wake mbapo kwa kiasi ya miaka 20 iliopita Zanzibar haikuwa na hata chuo kikuu kimoja na kupelekea wanaotaka kusoma kuenda nje ya Tanzania.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments: